Picha juu na Chini Wanafunzi wa shule
mbalimbali za msingi na sekondari jijini Dar wakiwa wamebeba mfano wa Njiwa
kuashiria Amani katika maadhimisho wakiandamana kuelekea ukumbi wa Karimjee
katika maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani leo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini
Dkt. Alberic Kacou akimkaribisha Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Amani
Duniani aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha-Rose
Migiro.
Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana
na Balozi wa Nigeria
nchini Tanzania Dr. Ishaya Nanjabu.
Dkt. Migiro akiteta jambo na Dkt. Kacou
wakati Balozi wa Nigeria Dr. Nanjabu akizungumza na mmoja wa maafisa wa jeshi
hapa nchini wakati wakisubiri maandamano ya Amani.
Dkt. Migiro sambamba na Dkt. Kacou
wakielekea kupokea maandamano ya Wanafunzi wa Shule mbalimbali jijini Dar katika
maadhimisho ya siku ya Amani Duniani.
Mgeni rasmi Dkt. Migiro (katikati), Dkt.
Kacou pamoja na Balozi wa Nigeria nchini Dr. Nanjabu (kushoto) wakiwa wamebeba
sanamu mfano wa ndege aina ya Njiwa ikiwa ni Ishara ya
Amani.
Mgeni rasmi Dkt. Asha-Rose Migiro akiimba
nyimbo za kuhamasisha Amani pamoja na washiriki wa maandamano ya siku Amani
Duniani.
Afisa Habari kutoka kitengo cha habari cha
Umoja wa Mataifa Stella Vuzo akitoa utambulisho wa meza kuu.Katikati ni Mgeni
rasmi Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha-Rose Migiro,
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou (wa pili kushoto),
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Right to Play Bw. Francis Rwiza
(kulia), Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Dr. Ishaya Nanjabu na Wa pili kulia
ni Program Manager wa Global Network of Religions for Children (GNRC) Bi.
Elizabeth Mwase.
Wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini
Dar wakati wa maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani yenye Kauli mbiu "AMANI ENDELEVU KWA UENDELEVU WA MASIHA YA
BAADAE".
Mmoja wa viongozi wa madhehebu ya Dini
kutoka BAKWATA akitoa sala wakati w ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Amani
Duniani leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dkt.
Alberic Kacou akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani
Duniani ambapo amerejea kusisitiza kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw.
Ban Ki-Moon katika ujumbe wake wa amani mwaka huu.
Amesema katika Siku ya Kimataifa ya Amani,
Umoja wa Mataifa unatoa wito wa kusitishwa kabisa kwa mapigano mahali mbalimbali
duniani kwa kuwa mapigano ya silaha yanashambulia mihimili muhimu ya maendeleo
endelevu.
Bw. Kacou pia ametumia fursa hiyo
kulipongeza Bunge la Tanzania kwa dhima yake ya kuhamasisha Utawala Bora na
kupiga vita ufisadi ili kuleta maendeleo ya taifa.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Amani
Duniani aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha-Rose Migiro
akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani leo jijini Dar es
Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine amesema Tanzania itaendelea kuwa mfano wa
jinsi demokrasi inavyofanya kazi katika ukanda wa Afrika
Mashariki.
Aidha amesema mchakato unaoendelea wa
mabadiliko ya katiba umewaweka wanaume na wanawake wa Tanzania katika nafasi ya
kuamua kuhusu kuimarisha manufaa ya Kidemokrasia, kuimarisha utawala bora na
haki za binadamu.
Pichani ni baadhi ya mabalozi
wanaowakilisha nchi zao pamoja na maafisa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini wakisiliza hotuba ya mgeni rasmi Dkt. Asha-Rose Migiro (hayupo
pichani).
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwamo
wawakilishi kutoka Serikalini, Mabalozi na Viongozi kutoka Ofisi za Kibalozi na
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za jijini Dar.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Airwing
Brenda Simon aliyeshiriki shindano la Insha ya Siku ya Amani
Duniani.
Mshindi wa Insha wa maadhimisho ya siku ya
Amani Duniani kutoka Shule ya Sekondari Kibasila akisoma Insha yake mbele ya
wageni waalikwa hawapo pichani.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la
Kiserikali la Right to Play Bw. Francis Rwiza akimkabidhi cheti pamoja na
zawadi mshindi wa Insha ya maadhimisho ya siku ya Amani Duniani mwanafunzi wa
shule ya msingi Airwing Brenda Simon.
Wanafunzi kutoka shule ya msingi Buguruni
Viziwi wakitoa burudani wakati wa sherehe za maadhimisho
hayo.
Dkt. Asha R0se Migiro akiimba pamoja na
wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar wakati akiondoka ukumbini
hapo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa
nchini Dkt.Alberic Kacou akimsindikiza mgeni rasmi Dkt. Asha-Rose Migiro baada
ya shereh za maadhimisho hayo.
Dkt. Asha-Rose Migiro akifanyiwa
mahojiano na vyombo vya habari nchini.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania
Dkt. Alberic Kacou akiteta jambo na baadhi ya mabalozi waliohudhuria sherehe za
maadhimisho ya siku ya Amani Duniani zilizofanyika katika ukumbi wa Karimjee
jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari kutoka kitengo cha habari cha
Umoja wa Mataifa Stella Vuzo (wa nne kushoto) pamoja na wadau wakifurahia
sherehe za maadhimisho ya siku ya Amani Duniani.
Na.Mwandishi wetu
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Dkt. Asha Rose Migiro amesema ili amani idumu nchini kuna ulazima wa
raslimali za nchi zitumika kwa maendeleo.
Migiro amesema amani iliyopo nchini ni ya
kujivunia na inahitaji kutunzwa na kuheshimiwa.
Amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku
ya Amani duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Dkt. Migiro amesema ili amani idumu ni
lazima iwepo mipango madhubuti ya kuhakikisha uchumi unakua kwa kila nchi na
kuhakikisha kwamba raslimali za nchi zinatumika vizuri ili kuleta
maendeleo.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na mabalozi
na baadhi ya viongozi wa serikali na wabunge.
Comments