MATUKIO YA MAUAJI: BARAZA LA UVCCM LAINYOSHEA KIDOLE CHADEMA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Ndugu Martine Shigela akichangia ajenda katika kikao cha Baraza la Umoja huo, (katikati) ni Makamu Mwenyekiti Ndugu Beno Malisa na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Mfaume Kizigo, wakiwa katika kikao cha Baraza hilo kililofanyika Jana tarehe 12 katika ukumbi wa sekretarieti maarufu kama (white house) uliopo Makao Makuu ya Chama, Dodoma.

 Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)  wakifuatilia hoja kutoka kwa mmoja miongoni mwa wajumbe katika mjadala wa kupitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya Umoja huo ngazi ya Mkoa na Taifa.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Taifa UVCCM, ambae pia ni Mjumbe Kikao Cha Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhwan J. Kikwete akichangia hoja katika kikao Cha Baraza hilo.

Na Suleyman Mwenda.

UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), wamemaliza kikao cha baraza la umoja huo ambapo wamejadili ajenda mbalimbali za msingi kuhusu Uchaguzi na pia wamejadili juu ya hali ya siasa nchini na mfululizo wa matukio ya uvunjifu wa amani na mauaji, ambapo wamekinyooshea kidole Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa  kuwa vinara wa matukio ya mauaji, kitu ambacho ni hatari kwa Taifa.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ya Katibu Mkuu, jengo la Mikutano (whitehouse) katika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi, Dodoma.
Alisema kuwa,kumekuwa na matukio ya mauaji kwenye mikutano ya chama hicho katika mikoa ya Singida, Igunga, Tabora, Morogoro na Iringa hali ambayo imekuwa ikitishia Usalama na Amani ya Nchi.

“Tunalaani Chadema kuwa vinara wa vurugu  zinazosababisha mauaji na kila  tukio  linapotokea  viongozi  wa Chadema wanakuwepo, hali inayoonyesha kuwa siasa wanazoendesha si za kistaarabu” alisema.

Alisema kuwa  Chadema wanachojenga ni hatari kwa Taifa  na pia hatari kwa Umoja wa Vijana pia na kama wana mapenzi ya kweli na watanzania waache siasa zinazasababisha mauaji mara kwa mara.

Katika hatua nyingine, Shigela amesema kuwa,Kikao cha baraza Kuu kilimalizika jana na kufanya maamuzi baada ya kujadili na kupitisha majina ya wagombea  na baadhi ya nafasi majina yatapelekwa halmashauri kuu ya taifa (NEC) ambacho ni chombo cha mwisho cha maamuzi katika Chama.

Amezitaja nafasi ambazo tayari zimetolewa maamuzi, kuwa ni nafasi ya mwakilishi mmoja kutoka UVCCM kwenda UWT, Mwakilishi mmoja kutoka UVCCM kwenda wazazi, Baraza Kuu taifa nafasi tano Zanzibar na nafasi tano Bara, na sasa orodha hiyo inaandaliwa ili majina ya waliochaguliwa yatangazwe rasmi.

Amesema kuwa,katika nafasi nyingine ikiwemo Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti tayari yamewekewa alama na yatapelekwa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC).

Pia amewataka wagombea ambao tayari wamefanyiwa uteuzi waache siasa za kuchafuana na zile za makundi.

Aidha alisema kuwa Mkutano Mkuu wa taifa unatarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 20, mwaka huu na kutaka wajumbe wote kuhakikisha wanafika Dodoma Oktoba 19.

Shigela amesema kuwa, Baraza kuu lilipata nafasi ya kuwapongeza vijana wa Jumuiya kwa kuthibitisha kuwa umoja huo ni tanuru la kuoka viongozi kwa baadhi yao kuteuliwa nafasi mbalimbali serikalini na kwenye Chama na kulitaka Baraza kuu kuzingatia mahitaji ya vijana ili wapate fursa zaidi za kugombea ili umoja huo uweze kupeleka sura nyingi za vijana ndani ya chama.

Pia alisema kuwa wametapa nafasi ya kuitafakari taarifa ya kazi nzuri ya Serikali kwa kuwawezesha vijana katika suala la kuwapatia elimu na kuwawekea mikakati ya miaka mitano ya kusaidia vijana.

Shigela aliitaka Serikali kuwa na mipango ya kudumu ili kuweza kudhibiti majanga mbalimbali yanayotokea hapa nchini k.v mafuriko, kuzama kwa meli, mauaji n.k.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI