MTAKATIFU TOM ATUPIWA VIRAGO YANGA
Saintfiet akisaini mkataba na Yanga Julai mwaka huu, kulia ni mwesigwa na kushoto ni Seif Ahmad 'Magari' |
Na Mahmoud
Zubeiry
KOCHA
Mbelgiji Tom Saintfiet amefukuzwa usiku huu, baada ya kutofautiana sera na
uongozi wa Yanga na sasa Fredy Felix Minziro, aliyekuwa Msaidizi wake, atakaimu
nafasi yake.
Habari
zaidi, kuhusu kufukuzwa kwa kocha huyo, Yanga itatoa taarifa rasmi kesho asubuhi
saa 3:00, makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani.
Mapema leo
mchana, uongozi wa Yanga ya Dar es Salaam, ulitangaza kuisimamisha kazi
Sekretarieti nzima ya klabu, akiwemo Katibu Celestine Mwesigwa na Ofisa Habari,
Louis Sendeu, kutokana na kile ilichoeleza utendaji
usioridhisha.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Makamu
Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema kwamba maamuzi hayo yamefuatia kikao
cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika tangu saa 5:30 leo hadi saa
9:30.
Wengine
wanaokumbwa na panga hilo ni Masoud Saad, aliyekuwa Ofisa Utawala, Philip
Chifuka aliyekuwa Mhasibu na Hafidh Saleh aliyekuwa Meneja ambaye anahamishiwa
kwenye majukumu mengine.
“Tumesitisha
mikataba ya sekretarieti nzima, pia tumefanya marekebisho, tumemtoa Meneja wa
timu na muda si mrefu tutamtangaza Meneja mwingie pamoja na sekretarieti
mpya,”alisema Sanga.
Aidha, Sanga
alisema Kocha Mbelgiji, Tom Saintfieti anapewa onyo kali kwa kuzungumza ovyo na
vyombo vya habari.
“Tumekwishakutana
naye mara kadhaa kumpa utaratibu wa kuzungumza na vyombo vya habari, sasa
tutamuandikia barua ya kumkumbusha wajibu wake na kuzingatia wajibu wake,
kutozungumza na vyombo vya habari
holela,”alisema.
Kwa ujumla
maamuzi haya yanakuja baada ya Yanga kuanza vibaya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, ikiambulia pointi moja tu katika mechi zake mbili za awali, kutokana na
sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumamosi
na Jumatano ikachapwa mabao 3-0 Morogoro Uwanja wa Jamhuri,
Morogoro.
Sasa beki wa
zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Lawrence Mwalusako
atakaimu nafasi ya Katibu wa klabu hiyo, kufuatia kusimamishwa kwa Celestine
Mwesigwa, wakati kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Sekilojo Johnson Chambua
atakuwa Meneja mpya wa klabu hiyo, akirithi mikoba ya Hafidh
Saleh.
Habari
kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba viongozi hao wapya watatangazwa wakati
wowote kuanzia sasa kurithi nafasi za viongozi walioondolewa madarakani,
kutokana na kile kilichoelezwa utendaji
usioridhisha.
Nafasi
nyingine za Mhasibu mpya, iliyoachwa wazi na Philip Chifuka itakuwa chini ya
dada mmoja, aliyetajwa kwa jina moja tu, Rose aliyekuwa akifanya kazi ofisi hiyo
kwa muda mrefu, wakati Msemaji wa klabu iliyoachwa wazi na Louis Sendeu,
inaelezwa atapewa mdogo wa mke wa Ridhiwani Kikwete, aliyehesabu kura za
Abdallah Bin Kleb katika uchaguzi mdogo wa klabu, Julai 14.
Saintfiet
amefungwa mechi mbili Yanga katika mechi 14 alizoiongoza timu hiyo tangu ajiunge
nayo, Julai mwaka huu, akirithi mikoba ya Mserbia, Kostadin Bozidar
Papic.
Katika mechi
hizo, zimo sita za Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame,
ambazo aliiwezesha Yanga kutwaa taji, ikipoteza mechi moja tu dhidi ya Atletico
ya Burundi.
REKODI
YA SAINTFIET YANGA
<!--[if !supportLists]-->1.
<!--[endif]-->Yanga Vs JKT Ruvu
(Kirafiki) 2-0
<!--[if !supportLists]-->2.
<!--[endif]-->Yanga Vs Atletico (Burundi, Kagame)
0-2
<!--[if !supportLists]-->3.
<!--[endif]-->Yanga Vs Waw Salam (Sudan, Kagame)
7-1
<!--[if !supportLists]-->4.
<!--[endif]-->Yanga Vs APR (Rwanda, Kagame)
2-0
<!--[if !supportLists]-->5.
<!--[endif]-->Yanga Vs Mafunzo (Z’bar, Kagame)
1-1 (5-3penalti)
<!--[if !supportLists]-->6.
<!--[endif]-->Yanga Vs APR (Rwanda, Kagame)
1-0
<!--[if !supportLists]-->7.
<!--[endif]-->Yanga Vs Azam
(Kagame) 2-0
<!--[if !supportLists]-->8.
<!--[endif]-->Yanga Vs African Lyon
(Kirafiki) 4-0
<!--[if !supportLists]-->9.
<!--[endif]-->Yanga Vs Rayon (Kirafiki,
Rwanda) 2-0
<!--[if !supportLists]-->10.
<!--[endif]-->Yanga Vs Polisi (Kirafiiki,
Rwanda) 2-1
<!--[if !supportLists]-->11.
<!--[endif]-->Yanga Vs Coastal Union
(Kirafiki) 2-1
<!--[if !supportLists]-->12.
<!--[endif]-->Yanga Vs Moro United
(Kirafiki) 4-0
<!--[if !supportLists]-->13.
<!--[endif]-->Yanga Vs Prisons (Ligi
Kuu) 0-0
<!--[if !supportLists]-->14.
<!--[endif]-->Yanga Vs Mtibwa (Ligi
Kuu) 0-3
Comments