NIPO SALAMA WADAU NASHUKURU KWA USHAURI PIA

Bw Francis Godwin
Napenda kuwashukuru wadau wote kwa kuendelea kuwa karibu nami hata kutaka kujua hatua kwa hatua na usalama wa maisha yangu, kiukweli Mungu anazidi kunipigania nipo sehemu salama na naendelea vema ,huku timu ya vijana wangu ikiendelea na kufanya kazi kama kawaida .kwani kabla ya kuondoka kwangu tulijipanga vema kuona hakuna tukio litakalokosekana katika mtandao huu toka pande zote za nchi kama ilivyokuwa hivyo hata kama mimi nitatendwa vibaya bado mtandao utaendelea kuweka mambo .
Nautambua mchango wenu wote mlioutoa hapa chini
Anonymous has left a new comment
on your post "NIMECHAGUA KUWA MKIMBIZI KATIKA KTK MKOA WANGU...":
Francis Godwin,kwanza ya yote Ubarikiwe mdogo wangu!Naamini kufuatia mauaji ya
ndugu yetu mpendwa Daudi Mwangosi,blog yako itasomwa sana tena na
wengi!Nakupongeza sana kwa moyo wangu wote kwa ujasiri mkubwa uliouonyesha
katika kipindi hiki kigumu sana katika maisha yako.Tumempoteza Daudi,lakini
ukweli ni kwamba Daudi ataendelea kubakia katika mioyo yetu na fikra zetu mpaka
mwisho wa uhai wetu.Picha za tukio zinaeleza kila kitu,mtu hahitaji maelezo ya
ziada.Nakupongeza kwa mara nyingine tena,kwa kukuhakikishia kwamba hupo peke
yako katika hili.Limewagusa wengi kwa huzuni kubwa!Ni unyama ambao wengi wetu
hatujapata kuushuhudia ukitokea katika nchi yetu iliyojaliwa udugu,maelewano na
amani,toka ilipopata uhuru mwaka 1961!Nakubaliana na wewe kwamba lazima uchuke
tahadhari kubwa hivi sasa kulinda uhai wako na ikiwezekana sio lazima watu
wajue umejificha wapi kwa sasa.Muda ukiruhusu,usisite kuuanika ukweli zaidi
kile kilichotokea muda mfupi tu kabla ya kifo cha Daudi Mwangosi.Zipo njia
nyingi za kuyaweka hadharani yaliyotokea ili ukweli uwasute wabaya na maadui wa
haki!tutaendelea kuwasiliana zaidi kupitia njia mbalimbali.Nifikishie pole
zangu kwa wanahabari wote wa Iringa na jamaa wote kwa jumla,na maalum kwa
wafiwa na ndugu wa karibu wa marehemu.Hakuna atakayeishi milele duniani,"siku
za binadamu zimehesabiwa",na malipo ni hapahapa duniani!Kaa kwa amani
Godwin,usiwaze sana,yote mwachie Mungu!

Chimbuko Letu has left a new
comment on your post "NIMECHAGUA KUWA MKIMBIZI KATIKA KTK MKOA WANGU...":
Pole sana Kaka
ni kweli unakuwa mtumwa kwenye Nchi yako kaka kwa kusema ukweli wa jambo ambalo
una uhuru nalo kuzungumza na jamii ikafahamu jamani,Jamani tunaelekea wapi
jamani?..... inauma sana sio siri

Anonymous has left a new comment
on your post "NIMECHAGUA KUWA MKIMBIZI KATIKA KTK MKOA WANGU...":
Pole sana mkuu kwa kuanza kufuatwafuatwa. Ni vema akatumbia kile kilichofanya
uondoke iringa. Usifiche ukweli kama Ulimboka. Ukweli ndio utakuweka huru.
Kama vipi nakushauri nenda Ubalozi wa nchi yoyote hapa Tanzania. Utapata
hifadhi nzuri na kamwe hutadhulika. Utakuwa umeliweka suala la kutishiwa maisha
yako mikononi mwa jumuiya ya Kimataifa. Unaweza kwenda ubalozi wa nchi za
kigeni hapa Bongo.Chanzo. FRANCIS GODWIN BLOG

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.