MAANDAMANO YA WANANCHI KUPINGA UWEPO WA RPC KAMUHANDA YAPIGWA STOP


Polisi wakiwa tayari eneo la tukio kuzuia maandamano ya wananchi wa Iringa Leo hii
/ Mbunge wa Iringa mjini kupitia chadema Peter Msigwa akizungumza na wananchi na wanahabari kuhusu kusitishwa kwa maandamano ya kupinga kuwepo kwa RPC Kamuhanda
Mbunge wa Iringa mjini Msigwa akitoka eneo la ofisi akielekea hospitali kwa matibabu ya mguu wake baada ya kusitishwa kwa maandamano

  
Mbunge wa Iringa mjini kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Peter Msigwa, akizungumza na wanachama na wapenzi wa chama hicho katika ofisi za Wilaya za chama hicho kuhusu kuahirishwa kwa maandamano ya amani  yaliyokuwa yafanyike siku ya leo kushinikiza kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda kujiuzulu kutokana na kifo cha mwandishi wa habari wa channel ten Daudi mwangosi kilichotokea tarehe 2 septemba mwaka huu.
Msigwa amesema kutokana na barua aliyoipata toka kwa zikitaka kusitisha maandamano hayo, aneleza barua inawataka kusitisha na kueleza kuwa sababu kubwa ni kwamba maandamano hayo hayataweza kuwa na polisi wa kusimamia na kukataza kufikia katika ofisi ya RPC  ambayo ni ofisi ya kiserikali.
Hata hivyo Msigwa ameeleza kuwa msimamo wao uko pale pale ila anajiandaa kujibu hoja za barua hiyo na kuwataka wananchi wawe na subira mpaka atakapowatangazia tena kuwepo kwa maandamano hayo ya amani.
Wakati huo huo wameonekana askari wakiwa katika magari yao kudhibiti wananchi kuandamana. Hali hiyo ilitokana na wananchi  hao kumiminika kwenye ofisi za Chadema mjini hapa kwa ajili ya kujiandaa maandamano.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.