WAZIRI WA UCHUKUZI DR.HARRISON MWAKYEMBE AKIWA NCHINI UJERUMANI
Waziri Harrison Mwakyembe akiwa na Balozi wa Tanzania Berlin Mhe. Ahmada R. Ngemera (kushoto) na Afisa wa Wizara ya mambo ya Nje, Ali Ubwa Mussa (Kulia).
…………………………………
Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe na ujumbe wake wapo Berlin kuanzia kuanzia tarehe 15 hadi 19 septemba, 2012. moja ya tukiomuhimu litakalofanyika huko ni ni kusainiwa kwa Mkataba wa Ushirikiano wa Usafiri wa Anga (Bilateral Air Services Agreement – BASA) baina ya nchi hizi mbili tarehe 17 Sept. Aidha, juzi tarehe 16 septema. Mhe. Waziri na ujumbe wake walitembelea maonyesho ya Kimaitaifa ya sekta ya Usafiri wa Anga yaliofanyika katika jiji la Berlin. Aidha kwa nyakati mbalimbali, Mhe Harrison Mwakyembe . na ujumbe wake walikutana na wafanyabiasha na wawekezaji mbalimbali hususani katika sekta ya usafiri (Anga, reli na meli).
Baada ya ziara ya ujeruman, ujumbe wa wataalam (tu) aliofatana nao Mhe. waziri utaelekea the Hague Uholanzi kwa ajili ya majadiliano mengine kuhusu usafiri wa anga tarehe 19 hadi 21 Septema. hata hivyo katika majadiliano hayo Mhe waziri Harrison Mwakyembe hatashiriki kwani atakuwa na majukumu mengine.
Mhe. Waziri Mwakyembe na ujumbe wake wakiwa katika Majadiliano na Uongozi wa Sekta ya Usafiri wa Anga nchini Ujerumani
Comments