YANGA YATAJA MABOSI WAPYA, YATAJA SABABU ZA KUMTIMUA MTAKATIFU TOM
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga akizungumza na Waandishi asubuhi hii. kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Tito Osoro |
MABOSI WAPYA; Kulia ni Oundo na kushoto Mwalusako |
Na
Mahmoud Zubeiry
KLABU ya
Yanga imetangaza rasmi kumfukuza Kocha wake Mkuu, Mbelgiji Tom Saintfiet na
nafasi yake atakaimu Msaidizi wake, Freddy Felix Minziro hadi hapo
atakapopatikana kocha mwingine.
Makamu
Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amesema asubuhi hii katika Mkutano na
Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani
kwamba, matokeo mabaya ndio yamefanya Saintfiet asitishiwe
mkataba.
Aidha, Sanga
alikanusha madai kwamba eti kocha huyo amefukuzwa baada ya kutofautiana na
Mwenyekiti wa klabu, Yussuf Manji.
“Timu
ilipokwenda Mbeya, ikatoka sare na Prisons aka
lalamikia huduma, lakini sisi
taarifa tulizozipata, yeye alikwenda kulewa na wachezaji. Kuna mapungufu mengine
mengi, ambayo hatuwezi kusema hadharani.
Kwa mfano
timu ilipotoka Mbeya, tulitaka iende moja kwa moja Morogoro, yeye akalazimisha
timu irudi Dar es Salaam, tena iende tena Morogoro. Wachezaji wakachoka sana na
hii tunaamini ilichangia hata kufungwa na Mtibwa.
Timu
iliporudi kutoka Morogoro, tukaamua iingie kambini, yeye akapinga akisema timu
kubwa kama Barcelona Ulaya, hazikai kambini, yaani anataka atupangie kazi sisi,
tukaona huyu mtu haendani na maadili ya uongozi na hatufai, tukaamua kusitisha
mkataba wake,” alisemsa Sanga.
Saintfiet
ameiongoza Yanga katika mechi 14 tu ndani ya siku 80 tangu ajiunge nayo Julai
mwaka huu, akirithi mikoba ya Mserbia, Kostadin Bozidar Papic na katika mechi
hizo amefungwa mbili tu, dhidi ya Mtibwa 3-0 na Atletico ya Burundi
2-0.
Katika mechi
hizo, zimo sita za Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame,
ambazo aliiwezesha Yanga kutwaa taji, ikipoteza mechi moja tu dhidi ya Atletico
ya Burundi.
Pamoja na
kufukuzwa kwa kocha, Yanga imemtangaza rasmi beki wa zamani wa Yanga na timu ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Lawrence Mwalusako kukaimu nafasi ya Katibu wa
klabu hiyo na Dennis Oundo kuwa kaimu Mkurugenzi wa Fedha na
Utawala.
Hatua hiyo,
inafuatia kusimamishwa kazi kwa Sekretarieti nzima ya klabu, akiwemo Katibu
Celestine Mwesigwa na Ofisa Habari, Louis Sendeu, kutokana na kile ilichoeleza
utendaji usioridhisha.
Wengine
waliokumbwa na panga hilo ni Masoud Saad, aliyekuwa Ofisa Utawala, Philip
Chifuka aliyekuwa Mhasibu na Hafidh Saleh aliyekuwa Meneja ambaye anahamishiwa
kwenye majukumu mengine.
Mbali na
Mwalusako na Oundo, kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Sekilojo Johnson Chambua
anatajwa kupewa nafasi ya Umeneja, wakati nafasi ya Msemaji wa klabu iliyoachwa
wazi na Louis Sendeu, inaelezwa atapewa mdogo wa mke wa Ridhiwani Kikwete,
aliyehesabu kura za Abdallah Bin Kleb katika uchaguzi mdogo wa klabu, Julai
14.Kwa hisani ya Bin Zubeiry Blog
Comments