LIGI YA MABINGWA ULAYA: AC MILAN, PSG, SCHALKE 04, ARSENAL, DORTMUND ZAFUZU 16 BORA
Hii ilikuwa ni mechi kati ya Anderlecht dhidi ya AC Milan, ambapo Milan ilishinda mabao 3-1
Jack Wilshere wa Arsenal akiifungia timu yake ilipoumana na Montpellier ya Ufaransa. Arsenal ilishinda 2-0
Hili lilikuwa ni pambano baina ya mabingwa wa 'Eredivise' Ajax ya
Uholanzi, dhidi ya mabingwa wa 'Bundesliga' Borussia Dortmund ya
Ujerumani. Dortmund ilishinda mabao 4-1
MONACO, Ufaransa
Mabingwa wa Bundesliga, Borussia Dortmund wamefuzu 16
bora kutokea kundi D kwa ushindi wa mabao 4-1 ugenini Amsterdam ArenA dhidi ya
wenyeji Ajax, huku Real Madrid wakiungana na Wajerumani hao baada ya sare dhidi
ya Man City
BEKI Philippe Mexes alifunga bao tamu akiwa amelipa mgopngo
lango la maadui kuipa AC Milan tiketi ya kufuzu hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya kwa ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Anderlecht.
Mfaransa huyo alifunga bao hilo kuongeza lile la ufunguzi la
Stephan El Shaarawy, kabla ya Alexandre Pato kupigilia msumari wa mwisho katika
jeneza za Wabelgiji hao.
Paris St-Germain imesonga hatua inayofuata kutokea kundi A,
huku Schalke na Arsenal wakitinga mtoano wa 16 bora kutokea kundi B.
Mabingwa wa Bundesliga, Borussia Dortmund wamefuzu 16 bora
kutokea kundi D kwa ushindi wa mabao 4-1 ugenini Amsterdam ArenA dhidi ya
wenyeji Ajax, huku Real Madrid wakiungana na Wajerumani hao baada ya sare dhidi
ya Man City.
Katika mechi za kundi A, Ezequiel Lavezzi alikuwa shujaa wa
PSG, akifunga bao moja kila kipindi kuipa klabu hiyo ya Ligue 1 ushindi wa 2-0 ugenini
dhidi ya Dynamo Kiev. Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, alikuwa mpishi mkuu wa
Lavezzi katika mechi hiyo.
Kwa ushindi huo, PSG chini ya Carlo Ancelotti kimesimama kwa
pointi moja nyuma ya vinara Porto, ambao walishafuzu mtoano wa 16 bora kabla
hata ya juzi kuichapa Dinamo Zagreb mabao 3-0. Zagreb sasa inaburuza mkia bila
pointi, huku Kiev ikifuzu Europa League.
Katika kundi la B, Christian Fuchs aliifunga bao pekee
dakika ya 13 kuipa Schalke 04 tiketi ya kufuzu mtoano kwa ushindi wa 1-0
nyumbani dhidi ya Olympiakos. Ushindi huo umewabakisha kileleni mwa kundi,
licha ya Arsenal, kushinda 2-0 dhidi ya Montpellier.
Schalke itaweza kumaliza kinara wa kundi hilo, kama itamudu
kuichapa Montpellier katika mtangane wa mwisho makundi, huku Olympiakos tayari
ikiwa na tiketi ya kufuzu Europa League kwa kushika nafasi ya tatu ya kundi
hilo.
Katika kundi C, licha ya PSG kushinda mabao mabao 3-1 dhidi
ya Anderlecht, Malaga ya Hispania imeendelea kubaki kileleni mwa kundi hilo,
licha ya kulazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya Zenit St Petersburg – ambayop
imeambulia kutinga katika Europa League.
Katika mitanange ya Kundi la Kifo la D, Robert Lewandowski aliifungia
mara mbili Borussia Dortmund na kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ajax.
Katika mechi hiyo, Marco Reus alifunga bao la ufunguzi,
kisha Mario Goetze kufunga la pili, huku Daniel Hoesen akifunga la kufutia
machozi la Ajax.
Real Madrid ilijikuta ikiambulia sare ya bao 1-1 Etihadi
yaliko makazi ya Manchester City na kujihakikishia nafasi ya pili ya kundi hilo.
Sare imeing’oa Man City katika michuano hiyo, ingawa inaweza
kufuzu Europa League, lakini kama tu itafanikiwa kuichapa Dortmund katika mechi
ya mwisho, huku ikiiombea mabaya Ajax itakapoumana na Madrid huko Bernabeu
katika mechi za mwisho.
Comments