MBUNGE WA WAWI ALIYEFIWA NA MKEWAKE JANA USIKU AFIKWA NA JANGA JINGINE MCHANA HUU!

Mbunge wa Wawi Pemba Hamad Rashid Mohamed,(katikati) akiwa na wenzake ambao walikuwa na madai mbalimbali Mahakamani dhidi ya Chama cha CUF wakiwa kwenye moja ya harakati zao za mapambano hayo, ambapo leo Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam imeyatupilia mbali madai hayo na kuhalalisha Mkutano wa baraza kuu la CUF uliotoa maamuzi ya kuwafukuza uwanachama. Picha ya Maktaba ya Raha za Pwani.
PAMOJA na kufikwa na msiba wa kufiwa na mkewake mdogo jana usiku Mbunge wa Wawi Hamadi Rasid Mohamed, leo hii amefikwa na tukio jingine la kuangushwa kwenye kesiyake yake na wenzake dhi ya Chama cha Wananchi CUF. Kwa mujibu wa taarifa zilizo sambazwa kwenye mitandao ya kijamii na Naibu katibu Mkuuwa chama Cha Wananchi CUF Tanzania bara Julius Mtatiro maamuzi hayo yametolewa mchana huu Mahakama kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam. Taarifa kamili ya naibu katibu mkuu huyo ni hii hapa;
TUMESHINDA KESI YA AWALI AMBAYO MHE. HAMAD RASHID NA WENZIE WALIKISHTAKI CHAMA.
Hukumu imemalizika muda so mrefu hapa mahakama kuu.
Hoja zote za akina Hamad Rashid zimetupiliwa mbali.
Mahakama imejiridhisha kwamba, amri ya mahakama kuu ya kusitisha kikao cha BARAZA KUU kilichowafukuza uanachama HR na wenzake wanne haikufikishwa kwa chama kwa hivyo kikao husika kilikuwa halali.

Hii ina maana kwamba OMBI la Hamad Rashid na mawakili wake kuwa WAJUMBE WOTE WA BARAZA KUU la CUF wafungwe jela kwa kukiuka amri ya mahakama limetupiliwa mbali.

Kesi ya msingi ambayo HR na wenzake waliifungua kupinga uhalali wa KAMATI YA MAADILI YA CHAMA itasikilizwa tarehe 28/01/2013 ambapo mawakili wa chama watapangiwa tarehe YA kuleta hoja za kutaka kesi ya msingi ifutwe kwa kuwa taratibu zote zilifuatwa na walifukuzwa kihalali na kwa kuzingatia katiba ya chama.

Chama chetu kimefurahishwa na uamuzi huu kwani unaonesha namna ambavyo hatukukurupuka.
Chama pia kinatoa pole kwa mhe. Hamad Rashid kwa kufiwa na mkewe mdogo jana, tutashiriki katika kutoa pole na mazishi pia. Tunaamini haya ya kimahakama yana nafasi yake na ya kibinadamu hayakwepeki. Chanzo; Raha za Pwani Blo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.