- Get link
- Other Apps
SERENGETI YAWAPA RAHA WATANZANIA
Mfungaji wa bao la Serengeti, Mudathir Yahya Abbas kushoto akishangilia huku akipongezwa na wenzake Joseph Kimwaga Lubasha na Ismail Adam Gambo. |
Kwa hisani ya Bongo Staz Blog
TIMU ya
taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo imeifunga 1-0
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Tatu
na ya mwisho kuwania tiketi ya kucheza Fainali za vijana wa umri huo Afrika
zitakazopigwa nchini Morocco mwakani.
Kwa matokeo
hayo, Serengeti sasa inahitaji hata sare yoyote katika mchezo wa marudiano wiki
mbili zijazo mjini Brazzaville ili kukata tiketi ya Morocco
mwakani.
Kwa ujumla
Serengeti walipigana katika mchezo wa leo, kwani wapinzani wao walionekana kuwa
bora na wenye uzoefu zaidi yao.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Miiro Nsubuga, aliyesaidiwa na Mark Ssongo,
Balikowa Ngobi na Ronnie Kalemba wote kutoka Uganda, hadi mapumziko Serengeti
walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililopatikana dakika ya
15.
Bao hilo
lilifungwa kwa shuti la mpira wa adhabu na beki Mudathir Yahya Abbas kutoka
umbali wa mita 22 na mpira kabla ya kutinga nyavuni ulimbabatiza beki mmoja wa
Kongo na kumpoteza njia kipa Ombandza Mpea Joe na kujaa
nyavuni.
Faulo hiyo
ilitokana na kiungo wa Serengeti, Hussein Twaha Ibrahim ‘Messi’kuangushwa na
beki Okombi Francis wakati akiwa analekea kwenye eneo la hatari la
Wakongo.
Baada ya bao
hilo, Wakongo walijaribu kuongeza jitihada kiuchezaji, lakini ukuta imara wa
Serengeti ulioongozwa na kipa Peter Manyika uliwazuia kusawazisha hadi dakika 45
za kipindi cha kwanza zinatimia.
Baada ya
mechi hiyo, kocha wa Serengeti Boys, Mdenmark, Jacob Michelsen aliwapongeza
vijana wake, lakini akasema bado wana kazi kubwa mbele
yao.
Kocha wa
Kongo, Mfaransa Eddie Hudanski alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 88, baada
ya awali kuonywa kwa kutoa lugha chafu, lakini
akarudia.
Refa Nsubuga
alitoa kadi moja tu ya njano kwa Issambey Lonvreve aliyeingia kipindi cha pili
kuchukua nafasi ya Ibara Vinny.
Tanzania; Peter Manyika Peter, Miza Kriston Abdallah, Mohamed
Hussein Mohamed, Ismail Adam Gambo, Miraj Adam Suleiman, Mudathir Yahya Abbas,
Mohamed Salum Haroub, Joseph Kimwaga Lubasha/Dickson Isaac Ambundo, Hussein
Twaha Ibrahim, Suleiman Hamisi Bofu/Tumaini Baraka Mosha na Farid Mussa
Shah.
Kongo
Brazzaville; Ombandza
Mpea Joe, Tmouele Ngampio, Mabiala Gharlevy, Okimbi Francis, Ondongo Boungena,
Ibra Vinny/Issambey Lonvreve, Binguila Handy, Obassi Ngatsongo, Mohendiki Brel,
Atoni Mavoungou na Biassadila Arei.
Comments