*WATANZANIA WAISHIO UJERUMANI KUFANYA PATI YA KUMUAGA MHE. BALOZI AHMADA NGEMERA


Watanzania waishio Ujerumani kufanya hafla ya kumuaga Mhe,Balozi Bw.Ahmada Ngemera ! Jumamosi 08-December 2012 mjini Berlin,Ujerumani.

Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) unaheshima kubwa kutarifu na kuwaomba watanzania wote wanaoishi ujerumani na jirani ya Ujerumani kuwa umoja wetu tunatarajia kufanya afla ya kumuaga Mheshimiwa balozi, Ahmada Ngemera,  ambaye anamaliza muda wake wa kufanya kazi.

Hafla hiyo itafanyika mjini Berlin siku ya Jumamosi tarehe 8.12.2012 .
Mhe. Balozi bwana Ahmada Ngemera amekua balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na watanzania wanaoishi ujerumani watamkumbuka daima Mheshimiwa Balozi Bw.Ahmada Ngemera kwa kuwa karibu sana na jamii ya watanzania,pia atakumbukwa kwa jitihada zake au kile ambacho watanzania
 wa ujerumani wanachokiita kuasisi Umoja na mshikamano wa watanzania nchi ujerumani,ambapo Mhe. Balozi, Ngemera na msaidizi wake Mhe.Bw.Ali Siwa wahamua kuhamasisha watanzania  waishio Ujerumani kuungana katika kila hali kuanzisha umoja wa mshikamano wa watanzania,kitu 
ambacho mabalozi wengi walishindwa kufanikiwa kufanya labda kwa sababu ya ukubwa wa nchi ya ujerumani wa watanzania wanaishi katika miji mbali mbali,lakini kazi hiyo ya kuwaungunganisha watanzania, Balozi Bw.Ahmada Ngemera na Msaidizi wake Bw.Ali Siwa walifanikiwa kuwafikia watanzania wote waishio Ujerumani na kuwashauri waanzishe umoja wa mshikimano,na matunda ya juhudi zao ndipo kukazaliwa Umoja wa waTanzania Ujerumani.(UTU)  Umoja ambao ni chombo cha watanzania wote ! chombo ambacho watanzania waishio ujerumani wanajivunia . 

UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO MSINGI WETU IMARA!
OMBI:
TUNAWAOMBA WATANZANIA WOTE ! NA MARAFIKI WOTE WA TANZANIA
AMBAO WANATAKA KUSHIRIKI KATIKA AFLA HII,
TUNAOMBA MTOE MCHANGO WA EURO 20.00 NA KWA WANAFUNZI EURO 10.00 TU
 kwa kupitia Account : Union of Tanzania in German e.V.
VR Bank Rosenheim-Chiemsee AG
Konto-No.: 59641   BLZ: 71160161
Verwendungszweck: „Kumuaga Mhe. Balozi Ngemera

Pia unaweza kuwasiliana na kamati.utu@googlemail.com
simu namba  +491734297997 au Katibu simu namba 01734744265

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI