BREAKING NEEEWZ!! RAIS WA MAKAPERA TANZANIA, ISSA KWISSA MWAIFUGE AJIUZULU UKAPERA AWAGEUKA WENZAKE GHAFLA NA KUOA RASMI
Rais
wa Makapera Tanzania, Issa Kwisa Mwaifuge, leo ameamua kuwageuka
wafuasi wake rasmi na kuvunja katiba ya kundi lake na kuamua kuuaga
ukapera rasmi na kumuoa Binti mrembo aliyewahi kushiriki shindano kubwa
la Miss Tanzania, 2004, Verdiana Kamugisha, ambao kwa pamoja wameamua
kumeremeta siku ya leo na kufunga ndoa yao katika Kanisa la Lutheran
lililopo mitaa ya Sinza jijini Dar es Salaam. Na hapa ni wakati wakiwa
katika sherehe ya ndoa yao inayoendelea muda huu katika Ukumbi wa
Msasani Makuni. Picha Zote na www.sufianimafoto.blogspot.com
Bwana Harusi, Issa Kwisa (kushoto) akisebeneka na Suleiman Semunyu, aliyekuwa akipokea zawadi ya keki kwa niaba ya ITV.
Maharusi, wakipozi kwa picha na wafanyakazi wa Star Tv, baada ya kuwakabidhi zawadi ya keki.
Hapa ilikuwa ni muda wa Kwaito……….
Sehemu ya wageni waalikwa…..
Wadau kutoka (kulia) ni James Range, Joseph Mpangala na Martine Mauya, wakipozi kwa picha mbele ya kamera ya Sufiaimafoto.
Baadhi
ya wafanyakazi wa ITV ambao ni wafanyakazi wenzake na Bwana Harusi,
wakipozi kwa picha, baada ya kukabidhiwa zawadi ya keki na Bwana harusi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Chanel Ten, wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kupokea zawadi ya Keki.
Salum
Mkambala, akisebeneka kwa staili yake wakati akielekea kupokea zawadi
ya keki kwa niaba ya wafanyakazi wenzake wa Chanel Ten.
Comments