RAIS - UTEUZI TASAF STEERING COMMITEE


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya TASAF (TASAF STEERING COMMITTEE) kwa kipindi cha miaka mitatu.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba 31, 2012 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo umeanza Desemba 20, 2012.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Bwana Peniel M. Lyimo – Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TASAF.
Wajumbe wa Kamati Tendaji ya TASAF walioteuliwa ni kama ifuatavyo:
(i)               Dkt. Khalid Salum Mohamed – Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.
(ii)            Bw. Amran Masoud Amran – Ofisa Mdhamini (Pemba), Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar.
(iii)         Bw. January R.L. Kayumbe – Idara ya Umwagiliaji, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
(iv)          Bi. Winfrida Annajoyce Nshangeki – Mkurugenzi Idara ya Serikali za Mitaa, TAMISEMI.
(v)             Bi. Nyancheghe Anna Konyo Nanai – Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu.
(vi)          Bw. Ally Msaki Ahmed – Mkurugenzi Msaidizi Soko la Ajira, Wizara ya Kazi na Ajira.
(vii)       Bi. Constansia Peter Gabuse – Mkurugenzi Msaidizi  Jinsia, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
(viii)    Bi. Ened A. Munthali – Mratibu wa Sera na Mipango, Ofisi ya Rais, Ikulu.
(ix)          Bi. Mariam Ally – Mchumi Mkuu, Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
(x)             Bw. Hussein Mativila – Mhandisi, Wizara ya Ujenzi
(xi)          Bw. Jerome J.R. Buretta – Kamishna Msaidizi, Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Uchumi.
(xii)       Bw. Zuberi Samataba – Mkurugenzi, Elimu ya Msingi, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
(xiii)    Bw. Abbass Kandoro – Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Desemba, 2012

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI