Afrika Kusini yaaga fainali za Afrika


Mchezaji wa Afrika Kusini
Afrika Kusini imebanduliwa nje ya mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika, baada ya kulazwa magoli matatu kwa moja kupitia mikwaju ya Penalti na Mali.

Timu hizo mbili zilitoshana nguvu ya kufungana bao moja kwa moja katika dakika tisini za kawaida na hata baada ya dakika zaidi thelathini kuongezwa hakuna aliyefanikiwa kuona lango la mwenziye na hivyo mechi hiyo kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Kinyume na matarajio ya wengi, wenyeji wa fainali hizo Afrika Kusini ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupiga mikwaju yake na kufanikiwa kupata mkwaju wa kwanza pekee.

Mali ilijibu kwa kufunga mikwaju mitatu na katika mkwaju wa kuamua ikiwa wataendelea, mkwaju uliopigwa na mchezaji wa Afrika kusini ulipaa juu ya goli na hivyo kuwapa Mali ushindi bila kupiga mkwaju zaidi.

Mali na Ghana tayari zimefuzu kwa nusu fainali ya mashindano hayo.

Washindi wengine wawili kuamuliwa katika mechi baina ya Nigeria na Ivory Coast na Togo na Burkina Faso siku ya Jumapili.
Goli la Afrika Kusini limefungwa katika dakika ya 31 na Tokelo Rantie.

Afrika Kusini ilifuzu kucheza robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ikiwa mshindi wa kwanza kutoka kundi A, huku Mali wakitokea kundi B wakiwa washindi wa pili.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.