AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU VYA SHILINGI MILIONI 9 KWA SHULE ZA SEKONDARI KAGERA

Toka kulia ni Ofisa Mauzo wa Airtel Kagera, Leonard Maige na Meneja Mauzo wa Kampuni ya Airtel wa mikoa ya Kagera na Kigoma, Peter Kimaro katikati wakikabidhi sehemu ya vitabu vya sekondari vya masomo ya sayansi kwa Ofisa Elimu wa shule za sekondari Kagera, Florian Kimolo ikiwa ni msaada uliotolewa na Airtel kwaajili ya shule za sekondari kanyeranyere, Kirushya na Nyamigogo za Kagera, Hafla ya Makabidhioano imefanyima katika shule ya sekondari  kanyeranyere ya wilaya ya Muleba -Kagera.Mwishoni mwa wiki. Airtel imekabidhi Vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 9Add caption

AddToka kulia ni Afisa Mauzo wa Airtel Kagera bw Leona Maige na Meneja mauzo wa kampuni ya Airtel wa mikoa ya kagera na kigoma bw. Peter Kimaro wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari kanyeranyere ya wilayani muleba mkoani kagera wakiwa wameshikiria vitabu vya sayansi na hisabati walivyokabidhiwa na kampuni ya Airtel mwishoni mwa wiki.Vitabu vilivyokabidhiwa vinathamani ya shilingi
milioni 9.
Shule za sekondari za kanyeranyere, Kirushya na Nyamigogo Kagera zakabithiwa vitabu hivyo Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa shule yetu imeendelea kutoa mchango wake katika sekta ya elimu ili kuboresha elimu, kuongeza idadi  na ufaulu wa wanafunzi wa sayansi na kupunguza uhaba wa vifaa vya kusomea mashuleni.  Airtel imefanya hivyo kwa kutoa msaada wa vitabu vya kufundishia katika shule 3 za sekondari zilizoko Mkoani Kagera mwishoni mwa wiki hii.

Shule zilizofaidika na msaada wa vitabu hivi ni pamoja na shule za sekondari za  Kanyeranyere iliyoko muleba, Kirushya wilayani Ngara pamoja na Nyamigogo iliyoko Biharamuro  kagera

Akiongea wakati wa halfa fupi ya kukabidhi vitabu vya masomo ya sayansi na hisabati  Afisa elimu wa shule za sekondari mkoani KageraFlorian Kimolo alisema" shule nyingi za sekondari katika mkoa wa Kagera zimekuwa na upungufu mkubwa wa vifaa vya kujifunzia nakufundishia sanjari na uhaba wa vifaa vya maabara na walimu. Kutokana na upungufu wa vitendea kazi katika shule mbalimbali za sekondari hapa nchini  tunaomba wadau  wa elimu kujitokeza katika kusaidia kulitatua tatizo hilo ili shule hizo ziweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Tunashukuru sana Airtel kwa mchango wao katika elimu na katika kuhakikisha tunapata wanafunzi wengi wa masomo ya sayansi na walimuwanapata vitabu vya kutosha katika kufundishia masomo haya na mwisho kupata ufaulu wa kiwango cha juu.

Naye Meneja  mauzo wa Airtel katika mikoa ya Kagera na Kigoma Peter Kimaro alisema " Airtel imejipanga kuendeleza ushirikiano na serikaliili kuisaidia wizara ya elimu kufikia malengo waliojiwekea ikiwemo upatikanaji wa vitabu mashule na kuongeza kiwango cha  ufaulu. Hadisasa kwa kupitia mradi wa " shule yetu tumeweza kufikia shule nyingi za sekondari nchini. Na nimatumaini yetu vitabu tunavyowakabidhi leovitaleta mabadiliko ya elimu kwa shule hizi na mkoa wa Kagera kwa ujumla.

Naye mkuu wa shule ya sekondari Kanyeranyere iliyoko wilyani Muleba mkoani Kagera alitoa shukurani kwa niaba ya walimu wakuu wa shule za sekondari za kanyeranyere, Kirushya na Nyamigogo na kusema, tunashukuru Airtel kwa kuzikumbuka shule za mkoani Kagera, tunaahidikuvitumia vizuri vitabu hivi ili kuleta ufanisi zaidi na maendeleo ya kitaaluma katika shule zetu.

Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia vitabu mashuleni, zaidi ya shule 900 za sekondari hapa nchini zimenufaika kupitia kampeni ya mradi wa kampuni ya simu za mkononi Airtel ujulikanao "Airtel  shule yetu"         

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.