DEREVA ALIYEGONGWA NA RAV 4 ASIMULIA , MWENYE GARI ASHINDWA KUAMINI ,WAZUNGU NAO WAFIKA KUSHANGAA

 Naibu meya  wa Manispaa ya Iringa Gravas Ndaki akishangaa ajali ya karne yenye maajabu makubwa kwa mkoa  wa Iringa  ,ajali  iliyotokea  usiku wa leo eneo la Hoteli ya kati (makosa) au CRDB ya  zamani katika barabara ya Iringa -Dodoma,hakuna majeruhi  wala aliyepoteza maisha
 Askari  wa usalama barabara  nao  washangaa kuona ajali  kama hii katikati ya mji
 Mmiliki  wa  gari  aina ya  RAV 4 iliyogonga gari na kulipanda juu akiwa haamini  kilichotokea
 
 Huyu ndie mmiliki wa RAV4 inasadikika ni mfanyakazi  wa Tanroads mkoa  wa Iringa
 Dereva  wa Taxi yenye namba  za usajili T 510 AYUKelvin Kaduma akiwa  salama kabisa
Wazungu ambao  ndio  wanatengeneza magari nao  wakifika  kushangaa ajali  hiyo ya maajabu 

Dereva  aliyegongwa na gari aina ya RAV 4 yenye namba T 319 AFLBw  Kalvin kaduma ambaye  alikuwa akiendesha Taxi yenye namba  T 510 AYU amejitokeza kuelezea  chanzo  cha ajali  hiyo na jinsi ambavyo alivyonusurika kifo.

Kaduma anasema  kuwa alishuhudia  gari hilo RAV 4  hiyo  ikija kwa mwendo wa kasi na ndipo alipoamua  kusimama ili  kushuhudia na ghafla alijikuta akifunikwa na RAV 4 hiyo.

Alisema  kuwa  RAV 4 hiyo  iliruka  ukingo la  barabara  ambao  una michongoma na kujengwa kwa  sementi na kutua  juu ya Taxi yake na kushindwa  kuendelea na  safari na kuwa  iwapo asingesimama kuona mtiti wa gari hilo basi dereva huyo wa RAV4 angekufa kwa  kugonga nyumba iliyopo jirani ambayo ina hoteli ya Hast Tast .

Hata  hivyo amesema hana mchumbuko  wowote na kuwa  dereva huyo wa RAV 4 kwa sasa anashikiliwa na  polisi baada ya  kushindwa  kukimbia kutokana na pombe. Kwa hisani Francis Godwin Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI