ETO'O ALIGOMA KUJA TANZANIA AKIHOFIA KIFO, AFICHUA SIRI NZITO JINSI MAISHA YAKE YALIVYO SHAKANI
MSHAMBULIAJI Samuel Eto’o amesema viongozi wa soka Cameroonian wanataka afe.
Nyota huyo wa zamani wa Barcelona na
Real Madrid alisema hayo katika mahojiano ya kwenye mtandao aliofanyiwa
nyumbani kwao, na kuweka bayana kwamba ameweka ulinzi mkali wa Polisi
nyumbani kwake kumlinda.
Nahodha huyo wa Cameroon, ambaye
ameshinda Tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika mara nne, amekuwa kwenye mgogoro
na Shirikisho la Soka la nchini mwake kwa muda sasa, ingawa mara ya
mwisho ilielezwa tofauti zao zimemalizwa.
Samuel Eto'o na Cameroon walishindwa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika
Kwa mujibu wa taarifa zilizofikia BIN
ZUBEIRY, Eto’o alipozungumza na jarida la Je Wanda alisema: ‘Viongozi wa
FCF wanataka kushambulia maisha yangu, wanataka kuniua.
‘Ninaishi na kundi la walinzi na mmoja
analala mbele ya mlango wangu. nafanya hivi siyo kwa sababu wizi, lakini
kwa usala wangu.’
Eto’o, ambaye sasa anachezea klabu
tajiri, Anzhi Makhachkala ya Urusi, amekuwa akiwashutumu mabosi hao wa
FCF kwa kushindwa kuwajibika na kuendekeza rushwa, na kwamba angependa
kupewa jezi ya kuchezea kutoka moja kwa moja kwa wasambazaji wa Puma,
kuliko chama cha soka.
Eto'o anasema analala walinzi kibao chumbani kwake
Alisema: ‘[Shirikisho] wamebwia fedha
zetu kwa muda mrefu kiasi cha kutosha. Badala ya kuongoza soka kwa
maslahi yao jumla, wanafikiria maslahi yao tu, kusafiri daraja la kwanza
na kufungua akaunti Ulaya.’
Wiki iliyopita, Eto’o na wachezaji
wengine 10 waligoma kuja Tanzania kuungana na timu yao ya taifa,
Indomitable Lions kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Taifa Stars,
wakisingizia majeruhi. Wamekosa tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika mwaka huu.
FCF bado haijajibu chochote kuhusu madai
ya Eto'o, ingawa wiki iliyopita, Ofisa mmoja mkubwa kumtuhumu nyota
huyo kuvuruga soka kwenye nchi hiyo.
Comments