Kamati ya Uchaguzi TFF, yatoa majina ya waliopitishwa kugombea nafasi mbalimbali TFF na Bodi ya Ligi Kuu
UCHAGUZI
WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
(TFF)
NA
TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD (TPL BOARD)
04/02/2013
Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawataarifu wananchi
wote kwamba baada ya kufanya usaili kwa waombaji uongozi wa TFF na
Tanzania Premier League Board (TPL Board), Kamati imefanya maamuzi
yafuatayo:
1. TANZANIA PREMIER LEAGUE
BOARD
(a) Waombaji
uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Kanuni za uendeshaji za TPL Board na
Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa nafasi walizoomba kama
ilivyoonyeshwa hapa chini:
NAFASI
INAYOGOMBEWA
|
S/N0.
|
JINA
|
MWENYEKITI WA
TPL BOARD
|
1.
|
Hamad
Yahya Juma
|
2.
|
Yusufali
Manji
| |
|
| |
MAKAMU
MWENYEKITI WA TPL BOARD
|
1.
|
Said
Muhammad Said Abeid (Kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti
vyake)
|
MJUMBE
–KAMATI YA UENDESHAJI (Management Committee)
|
1.
|
Kazimoto
Miraji Muzo
|
|
2.
|
Omary
Khatibu Mwindadi
|
(b) Mwombaji
uongozi Ndg. Christopher Peter Lunkombe hakukidhi matakwa ya Kanuni za
uendeshaji za TPL Board Ibara
ya 28(2) kwa
kuwa cheti chake cha Elimu ya Sekondari kina utata. Kamati ya Uchaguzi ya TFF
imemwondoa kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya uendeshaji (Management
Committee) ya TPL Board.
2. SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
(a) Waombaji
uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za
TFF. Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa nafasi walizoomba kama
ilivyoonyeshwa hapa chini:
NAFASI
|
S/No.
|
JINA
|
RAIS
WA TFF
|
1.
|
Athumani
Jumanne Nyamlani
|
2.
|
Jamal
Emily Malinzi
| |
MAKAMU WA RAIS
WA TFF
|
|
|
2.
|
Ramadhan
Omar Nassib
| |
3.
|
Wallace
Karia
| |
MJUMBE
WA KAMATI YA
UTENDAJI
–
Kanda ya 1
(Kagera, Geita)
|
|
|
1.
|
Kalilo
Samson
| |
2.
|
Salum
Hamis Umande Chama
| |
|
| |
Kanda ya 2
(Mwanza, Mara)
|
1.
|
Jumbe
Oddessa Magati
|
2.
|
Mugisha
Galibona
| |
3.
|
Samwel
Nyalla
| |
4.
|
Vedastus
F.K Lufano
| |
|
| |
Kanda ya 3
(Shinyanga, Simiyu)
|
1.
|
Epaphra
Swai
|
|
| |
Kanda ya 4
(Arusha, Manyara)
|
|
|
1.
|
Elley
Simon Mbise
| |
2.
|
Omar
Walii Ali
| |
|
| |
Kanda ya 5
(Tabora, Kigoma)
|
1.
|
Ahmed
Idd Mgoyi
|
2.
|
Yusuf
Hamis Kitumbo
| |
|
| |
Kanda ya 6
(Rukwa, Katavi)
|
|
|
1.
|
Blassy
Mghube Kiondo
| |
2.
|
Seleman
Bandiho Kameya (Kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti
vyake)
| |
|
| |
Kanda ya 7
(Iringa, Mbeya)
|
1.
|
David
Samson Lugenge
|
2.
|
John
Exavery M. Kiteve
| |
3.
|
Lusekelo
E. Mwanjala
| |
|
| |
Kanda ya 8
(Ruvuma, Njombe)
|
1.
|
James
Patrick Mhagama
|
2.
|
Stanley W. D
Lugenge
| |
|
| |
Kanda ya 9
(Mtwara, Lindi)
|
1.
|
Athuman
Kingome Kambi
|
2.
|
Francis
Kumba Ndulane
| |
3.
|
Zafarani
Mzee Damoder
| |
|
| |
Kanda ya 10
(Dodoma, Singida)
|
1.
|
Hussein
Zuberi Mwamba
|
2.
|
Stewart
Ernest Masima
| |
|
| |
Kanda ya 11
(Morogoro, Pwani)
|
|
|
1.
|
Riziki
Juma Majala
| |
2.
|
Twahil
Twaha Njoki
| |
|
| |
Kanda
ya 12 (Kilimanjaro, Tanga)
|
1.
|
Davis Elisa
Mosha
|
2.
|
Khalid
Abdallah Mohamed
| |
3.
|
Kusianga
Mohamed Kiata
| |
|
| |
Kanda ya 13
(Dar es salaam)
|
1.
|
Alex
Crispine Kamuzelya
|
2.
|
Juma
Abbas Pinto
| |
3.
|
Muhsin
Said Balhabou
|
(b) Waombaji
uongozi wafuatao hawakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za
TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imewaondoa kugombea nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:
(i) Ndg. Omary
Mussa Nkwarulo anayeonba
kugombea nafasi ya Rais wa
TFF hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni
za Uchaguzi za TFF Ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu
majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na
malengo ya TFF.
(ii) Ndg. Michael
Richard Wambura anayeonba
kugombea nafasi ya Makamu wa Rais
wa TFF hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni
za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kuwa Ndg. Michael Wambura alifungua kesi ya
madai namba 100 ya 2010 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam
dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba akiwa ni mwanachama wa Klabu ya Simba,
kinyume na Katiba ya Klabu ya Simba. Kwa kufanya hivyo, Ndg. Michael Wambura
alivunja Katiba ya Klabu
ya Simba, alikiuka Katiba ya TFF na Katiba ya FIFA.
(iii) Pia Kamati
inaheshimu maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Rufaa ya TFF kuhusu uchaguzi mwaka
2008 kwamba Bw. Michael R. Wambura hakukidhi matakwa ya Ibara ya 29(7) ya Katiba
ya TFF na Ibara ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kwa mujibu wa Katiba
ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF, Kamati ya
Uchaguzi ya TFF haina mamlaka ya kubadilisha maamuzi yaliyofikiwa na Kamati hiyo
ya Rufaa. Maamuzi hayo yanaweza tu
kubadilishwa na Mahakama ya usuluhishi wa masuala ya michezo (CAS).
(iv) Ndg. Abdallah
Hussein Musa anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 1 (Kagera,
Geita) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni
za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu
majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na
malengo ya TFF.
(v) Ndg. Mbasha
Matutu anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 3 (Shinyanga,
Simiyu) hakukidhi
matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni
za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa aliingilia mchakato wa Uchaguzi kwa
kushirikiana na waweka pingamizi dhidi ya mgombea mwenzake.
(vi) Ndg. Charles
Mugondo anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 4 (Arusha,
Manyara) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni
za Uchaguzi za TFF kwa
kuwa vyeti vyake vya Elimu ya Sekondari na cheti cha Ualimu vina
utata.
(vii) Ndg. Ayubu
Nyaulingo anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 6 (Rukwa,
Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni
za Uchaguzi za TFF ibara ya 3 inayotaka
awe na uzoefu wa
uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) na
pia hakukidhi
Ibara ya 9(7) kwa
kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba
na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.
(viii) Ndg. Nazarius
A.M Kilungeja anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 6 (Rukwa,
Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni
za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa amekuwa sehemu ya migogoro ya muda
mrefu mkoani Rukwa.
(ix) Ndg. Eliud
Peter Mvella anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 7 (Iringa,
Mbeya) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni
za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mwaminifu kwa kukiuka uamuzi wa
pamoja wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuhusu
mabadiliko ya Katiba.
(x) Ndg. Farid
Nahdi anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 11(Morogoro,
Pwani) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni
za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(2) na (7) kwa kuwa maelezo ya umri wake na vyeti
vya elimu havikubaliani.
(xi) Ndg.
Hassan Othuman Hassan anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
Kupitia Kanda Na. 11 (Morogoro,
Pwani) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 11(5) kwa
kuwa hakuhudhuria
usaili.
(xii) Ndg. Omary
Isack Abdulkadir anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es
salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa
kuwa alikaidi
maagizo ya TFF ya kuahirisha uchaguzi wa chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu
Tanzania (FRAT)
na maagizo ya TFF kwa kuwa alienguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi wa FRAT kwa
kutotimiza matakwa ya Kanuni za uchaguzi za wanachama wa
TFF.
(xiii) Ndg. Shafii
Kajuna Dauda anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es
salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa
kuwa si mkweli: aliposhindwa kwenye uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Dar es salaam (DRFA) alipotosha umma kuhusu ushiriki wake kwenye uchaguzi huo na
mchakato mzima wa uchaguzi. Pia hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF na majukumu ya
Kamati ya Utendaji ya TFF.
3. Usaili
uliofanyika kwa waombaji uongozi ulizingatia pia taarifa zilizoifikia Kamati ya
Uchaguzi ya TFF kupitia pingamizi zilizowasilishwa dhidi ya waombaji uongozi wa
TFF na TPL Board.
4. Uchaguzi
wa TPL Board utafanyika tarehe 22 Februari 2013, na Uchaguzi wa TFF utafanyika
tarehe 24 Februari 2013 jijini Dar es salaam.
Deogratias
Lyatto
MWENYEKITI
Comments