KIJUE CHAMA CHA KUTETEA HAKI ZA WANAUME TANZANIA(TAMRA)
KATIBU WA UHAMASISHAJI WA TAMRA TAIFA BWANA HATIBU MGEJA AKIWA NA MWEKA
HAZINA WA TAMRA TAIFA BWANA JUMA KOMBO
TANZANIA MEN’S RIGHTS ASSOCIATION
CHAMA CHA KUTETEA HAKI ZA WANAUME TANZANIA
”TAMRA”
Equal treatments for all
UTANGULIZI
TAMRA ni Asasi ya kiraia iliyoanzishwa na wanaume wa Tanzania kwa
lengo la kutoa msaada wa Kisheria pamoja na Elimu ya Haki na Wajibu
katika mahusiano ya kindoa kati ya mwanamke na mwanaume.
Kuanzishwa kwa asasi hii kumekuja katika kipindi hiki baada ya tafiti mbalimbali kuonyesha kuwa wapo wanaume wengi
wanaofanyiwa vitendo vya ukatili katika masuala ya ndoa kwa kunyimwa
haki zao za kindoa kutupiwa virago pindi mwanamke anapoamua kumchoka
mwanamme kufuatana na kukosa kipato, kupungukiwa nguvu za kiume na mambo
kama hayo , jambo ambalo limeonekana kuwa ni chanzo cha migogoro katika
ndoa inayosababisha ongezeko la watoto wanaoishi bila wazazi wa pande
zote mbili yaani [ Baba na Mama] huku hali hii ikiigharimu jamii na wanandoa kupigana na kusababisha majeraha na mauaji katika jamii.
Si
hivyo tu Mwanamme wa Tanzania amekuwa ni mvumilivu kwa vile amekuwa
akitendewa mambo yote haya bila kuwa na chombo cha kukemea vitendo hivi
jambo lililotoa ushawishi kwa waanzilishi wa chama hiki kupata uchungu
na hatimaye kuamua kuanzisha Asasi hii.
Muda mrefu mwanaume wa Tanzania hakupata wapi pa kwenda kupata msaada wa kisheria, imefika wakati wanaume kuwa na chama
cha kuwatetea dhidi ya unyanyasaji kutoka kwa wake zao katika nyanja
mbali mbali ikiwemo mambo ya ndoa,urithi wa mali kwa wagane, pamoja na
ulezi wa watoto.
TAMRA kinaenda mbali katika kuelimisha wanaume juu ya haki zao za
msingi pamoja na kuwaelimisha juu ya wajibu wao kama baba katika
kuitunza familia yake,kuondoa mfumo dume na mfumo jike, kupiga vita
unyanyasaji kwa mke na watoto,urithi wa mali kwa wajane na wagane pamoja
na kulea watoto kabla na baada ya kufariki kwa wanandoa.
Jina la asasi: Asasi hii itajulikana kuwa ni Chama
cha kutetea haki za wanaume Tanzania/Tanzania Men’s Rights Association
kwa kifupi TAMRA
(1) Kuanzishwa kwa TAMRA:
Asasi ya TAMRA ilianzishwa 01/05/2012
(2) Makao Makuu.
Makao
makuu ya TAMRA yatakuwa katika Mtaa wa Mpakani ‘A”Kijito Nyama Jijini
Dar Es Salaam kituo cha Afrika sana Nyumba Block namba 45.
vile vile kutakuwa na ofisi ndogo ya Makao Makuu Jijini MWANZA
(3) Anuani ya Chama ni. Chama Cha Kutetea Haki za Wanaume Tanzania.
S.L.P 60065
Dar Es Salaam - Tanzania
Simu: Mwenyekiti TAMRA TAIFA +255 784 203 556
Katibu Mkuu TAMRA TAIFA +255 787 565 533
Baruapepe:tamratanzania@gmail.com
Blog: yetu ni www.tamratanzania.blogspot.com
TAFSIRI
“TAMRA” itamaanisha ni TANZANIA MEN’S RIGHTS ASSOCIATION.
KUTAKUWA NA VIONGOZI WAFUATAO WA TAMRA
· Kutakuwa na Mwenyekiti wa TAMRA Taifa.
· Katibu mkuu wa TAMRA Taifa.
· Mweka Hazina wa TAMRA Taifa.
· Katibu wa Uhamasishaji wa TAMRA Taifa.
· Wajumbe wa Bodi ya TAMRA
KAZI ZA TAMRA.
TAMRA itakuwa na kazi zifuafuatazo:
(1) Kutetea wanaume dhidi ya unyanyaswaji katika ndoa.
(2) Kutoa elimu juu haki za Wanamme
(3) Kuwaelimisha wanamme kuondokana na mfumo dume/jike.
(4) Kuelimisha wanaume kuhusu haki na usawa kati ya mwanamme na mwanamke katika kutoa maamuzi kwa mambo mbalimbali ya kifamilia, kisiasa na kiuchumi.
(5) Umiliki wa mali katika familia.
(6) Haki ya kushiriki na kufurahia ndoa.
(7) Kuelimisha jamii juu ya Haki ya kumiliki mali kwa pamoja kabla na baada ya kifo cha mmoja wa wanandoa.
(8) Kuelimisha wanandoa kuhusu Haki na wajibu wa kuheshimiwa na kupendwa kwa kila mwanandoa kama ilivyo katika maandiko matakatifu bila kuathiri itikadi za dini.
(9) Kuhakikisha kwamba TAMRA inashirikiana na taasisi
za kutetea haki za wanawake ili kuondoa imani potofu dhidi ya mwanamme
ili kujenga mahusiano mazuri katika familia badala ya kuchochea uhasama
kwa kumkandamiza mwanamme kuwa ndiyo chanzo cha migogoro ndani ya
familia.
10.kuhakikisha
kuwa kuna usawa na uhuru wa kujieleza pindi mashauri ya ndoa
yanapopelekwa katika vituo vya Polisi kwa uchunguzi na hatimaye hatua ya
kupelekwa katika vyombo vya maamuzi.
11.Kuhakikisha kuwa wapo Mawakili wa kutosha panapotokea mashauri katika Mahakama watakaotetea Haki za Wanaume ili kuhakikisha Haki inatendeka
MALENGO YA TAMRA.
TAMRA itakuwa na malengo kama ifuatavyo:-
(1) Kupigania Haki za mwanaume katika masuala mbalimbali ikiwamemo kulinda na kudumisha ndoa.
(2) Kulinda Haki ya mwanaume ngazi ya familia ,kitaifa na kimataifa.
(3) Kuelimisha waathirika wa unyanyasaji
(4) Kutoa msaada wa kisheria Bure kwa kutumia mawakili wa TAMRA.
(5) Kutoa
elimu ya Afya na malezi ya mtoto wa kiume ili akue katika maadili
yanayozingatia haki sawa kwa wote kuondoa dhana ya mfumo dume.
(6) Kutoa elimu juu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa yasiyokuwa na tiba ikiwamo Ukimwi (HIV/AIDS).
(7) Kutoa elimu na mafunzo kwa wanamme ili kuwafundisha ujasiria mali kuondoa utegemezi .
(8) Kufanya upatanishi na usuluhishi kwa wanandoa kwa kuzingatia mila,Desturi,Dini pamoja na sheria za Nchi.
(9) Kutoa elimu kwa wanaume kukubali mabadiliko ya mwili kufuatana na umri kuwa mkubwa kati ya mwanamme na mwanamke.
10 Kulinda Haki za kila raia bila kujali itikadi za dini, rangi, kabila jinsia na taifa.
11 Kutoa Elimu ya uraia.
11 Kushirikiana na serikali na taasisi mbalimbali za kimataifa katika maadhimisho ya siku ya mwanamme Duniani ikiwemo kuandaa sherehe hizo kitaifa kufuatana na kalenda ya kimataifa kila mwaka.
12 Kutoa misaada kwa makundi ya wasiojiweza yatima,
wazee,wagonjwa ,wakimbizi majeruhi wa ajari, majanga kama
njaa,mafuriko, shule au kujenga majengo ya kutoa huduma za afya na elimu
kulinda na kutunza mazingira kuangalia chaguzi ndani na nje ya
Tanzania.
USIKOSE
KUSIKILIZA KIPINDI MAALUM KATIKA RADIO NURU FM SIKU YA JUMAMOSI TAREHE
9 KITAKACHORUSHWA KUANZIA MIDA YA SAA 3.20 -4.00 USIKU TUTAKUWA NA
MWANASHERIA WA TAMRA BW.BENY SHABAKAKI
WAWEZA SIKILIZA LIVE HAPA WWW.FRANCISGODWIN.BLOGSPOT.COM
Comments