kinana akamilisha ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilaya ya kakonko na kibondo mkoani kigoma.
Katibu
Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelekezo mafupi
kuhusiana na bwawa la umwagiliaji kutoka kwa Injinia wa maji mkoa wa
Kigoma,Elinatha Elisha (haonekani pichani).Kinana amefanya ziara ya
kuutembelea mradi huo wa umwagiliaji katika kijiji cha Nyendara,Wilayani Kibondo mkoani Kigoma akiwa ameambatana na wajumbe wake wa chama cha CCM.
Katibu
Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelekezo mafupi ya
mitambo ya umwagiliaji kutoka kwa Injinia wa maji mkoa wa
Kigoma,Elinatha Elisha.Kinana amefanya ziara ya kuutembelea mradi huo wa
umwagiliaji katika kijiji cha Nyendara,Wilayani Kibondo mkoani Kigoma.
Sehemu ya mradi wa Bwawa la umwagiliaji,ambalo Katibu
Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana alitembelea na kujionea
maendeleo yake,kwa mujibu wa Injinia kutoka Ofisi ya Umwagiliaji kanda
ya Magharibi mkoani Tabora,Bwa.Bahati Balekele alieleza manufaa ya
Bwawa hilo kwa wakazi wa eneo hilo.alisema kuwa litasaidia katika
matumizi ya Kilimo cha Umwagiliaji,Matumizi ya mifugo pamoja na matumizi
ya majumbani.
Katibu Mkuu
wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya
wanakijiji Nyendara,alipokwenda kukagua mradi wa bwawa la Umwagiliaji la
Nyendara
Meneja wa kituo cha uzalishaji Umeme Wilaya ya Kibondo,Damson Lupenza akifafanua jambo mbele ya Katibu
Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana na wajumbe wake waliofika
eneo hilo kwa ajili kukagua maendeleo ya mradi huo wa Umeme.
Katibu Mkuu
wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na
Wafanyakazi wa kituo kinachozalisha umeme Wilaya ya Kibondo.
Mmoja wa mafundi wa kituo cha
kuzalisha umeme,Omary Mwinyimkuu akitoa maelezo mafupi kwa Katibu Mkuu
wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana (pichani kati),alipokwenda
kutembelea mradi wa Umeme,kijiji cha Twabangondozi,Wilayani Kibondo
akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu kichama wilayani
humo akiwemo mkuu wa Wilaya,Mh Venance Mwamoto
Comments