MAMA SALMA AWAFUNDA WANAFUNZI WA KIKE MKOANI RUKWA

Na Anna Nkinda – Sumbawanga
Watoto wa kike nchini wametakiwa kuepukana na vishawishi vya chips Kuku, lifti, simu za mkononi na zawadi za aina mbalimbali wanazorubuniwa nazo  kwani vitu hivyo havina nia njema ya  kumkomboa msichana kielimu , kijamii na kiuchumi  zaidi ya kumuharibia mpango mzima wa maisha yake.

Onyo hilo limetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanafunzi wa kike zaidi ya 1000 kutoka shule mbalimbali za mkoa wa Rukwa  katika viwanja vya shule ya Sekondari ya wasichana ya mtakatifu Theresia iliyopo mjini Sumbawanga.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kwamba watoto wengi wa kike wanashindwa kumaliza masomo na kufikia malengo kutokana na changamoto  zinazowakabili ambazo nyingi siyo za kitaaluma japo zinaathali nyingi kitaaluma , kiafya na kimaendeleo.

“Tunafahamu kuwa wanafunzi wengi hupata vishawishi ambavyo huwapelekea kupoteza umakini, muelekeo na kuwa watoro, kupata ujauzito, maambukizi ya Ukimwi na hatimaye kupoteza fursa hii adimu na adhimu ya elimu ya Sekondari na dira ya maisha yao. Ni muhimu kujidhatiti na kujiepusha na mitego, vishawishi na matendo yanayoweza kusababisha matatizo haya.

Msikubali vishawishi kwani peremende ya dakika si sawa na asali ya maisha.

Iweje uridhie kuuharibu mpango wa maisha yakokwa kitu cha mara moja? Licha tu ya kuwa atakayehusika na kosa la kukupa mimba anapaswa kushtakiwa kisheria, lakini kwako wewe ni hatari kiafya  kwani kushika mimba ukiwa na umri mdogo unahatarisha maisha yako wakati wa kujifungua. 

Asilimia ishirini ya vifo vya akina mama wajawazito hutokana na uzazi katika umri mdogo”, alisema Mama Kikwete.

Aidha Mama Kikwepi pia aliwataka wanafunzi hao kuwatii wazazi wao,kusoma kwa bidii na kujiamini kwamba wanaweza kwani chochote anachoweza kufanya mtoto wa kiume kitaaluma na halikadhalika mtoto wa kike anaweza kukifanya hivyo basi wasome  zaidi masomo ya sayansi na hisabati kama watoto wa kiume.
Akisoma taarifa ya shule ya Sekondari ya wasichana ya Mtakatifu Theresia Sr. Beatrice Cromweli ambaye ni mwalimu alisema kuwa shule hiyo ilianzishwa na shirika la masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika Jimbo la Sumbawanga mwaka 2007 ikiwa na wanafunzi 85 na hadi sasa kuna wanafunzi 489 na walimu 16.

Alisema kuwa lengo kuu la kuanzishwa kwa shule hiyo ni kuwaendeleza watoto wa kike kielimu na kimaadili ili kuwakomboa katika unyanyasaji dhidi ya mwanamke na hivyo kuwapa uwezo wa kujitambua, kujiamini na kufanya maamuzi sahihi katika maisha yao.

Sr. Cromweli alisema,“Shule yetu imefanikiwa kuongeza idadi ya wanafunzi kila mwaka hii hutokana na ongezeko la vyumba vya madarasa, mabweni ya kulala, vifaa vya kufundishia, walimu na vitendea kazi mbalimbali na ufaulu mzuri wa wanafunzi katika mitihani ya kidato cha nne”.

Alizitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni ukosefu wa vifaa vya maktaba ya kisasa kwani  ujenzi wa jengo  hilo ambalo halijaanza kutumika kikamilifu kutokana na ukosefu wa vitabu, meza, viti na kompyuta umeshakamilika, jengo la bwalo la chakula na ukumbi wa mikutano bado halijakamilika kwani halina meza na viti na uhaba wa vifaa vya maabara ambavyo vinawafanya wanafunzi kutofanya majaribio ya kuridhisha.

Mkoa wa Rukwa umekuwa ukikabiliwa na changamoto ya  kushuka kwa kiwango cha elimu hasa kwa mtoto wa kike , karibu asilimia 39 ya watoto hao huacha shule kabla ya kumaliza elimu ya  Sekondari kutokana na tatizo la utoro, ujauzito na wazazi kutotilia maanani suala la elimu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.