MAMA SALMA KIKWETE AONGOZA HAFLA YA KUCHANGIA WANAWAKE WENYE MATATIZO YA AFYA KIASI CHA SH. M. 142 ZAPATIKANA
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Montage (iliyoandaa hafla hiyo),Teddy Mapunda
akimpa zawadi ya heshima Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete mara baada ya
kuifanikisha vyema tafrija hiyo maalum ya harambee ya kuchangisha fedha
kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini
kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,iliyofanyika jioni ya leo kwenye
Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam,aidha katika tafrija hiyo
iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Montage (iliyoandaa hafla hiyo),Teddy Mapunda
pichani kushoto akizungumza machache mbele ya meza kuu kabla ya kumpa
zawadi ya heshima Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete mara baada ya kuifanikisha
vyema tafrija hiyo maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya
kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa
Montage Charity Ball,iliyofanyika jioni ya leo kwenye Hoteli ya
Serena,jijini Dar es Salaam,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana
kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana.Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal.
Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi Bwa.Charles Stith ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia $ 10,000 kwenye hafla ya kukusanya
kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia
matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali,Anaeshuhudia pichani kulia ni Mke wa Makamu wa Rais,Mama
Asha Bilal,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi
milioni 142 na laki tano zimepatikana usiku huu,ndani ya hoteli ya
Serena,jijini Dar.
Mke
wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal pichani kulia akizungumza
machache,ambaye pia alichangia kiasi cha shilingi Milioni mbili katika
hafla hiyo.
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa pongezi na Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal kwa kuchangia kwake.
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa pongezi na kumkabidhi cheti cha heshima Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal kwa kuchangia kwake.
Mgeni Rasmi,Mke
wa Rais, Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti cha heshim mmoja wa
watangazaji wa kipindi cha Powerbreakfast kutoka Clouds FM,Said Bonge
a.k.a Bonge Barabarani ambaye pia alichangia kiasi cha shilingi laki
tisa.
Makofi ya pongezi na shukurani kwa Bonge Barabarani yakipigwa.
Mgeni
Rasmi,Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza machache mbele ya
wageni waalikwa (hawapo pichani) mara baada ya kuifanikisha hafla hiyo
kwa kiasi kikubwa.
Mmoja wa Waratibu wa hafla ya Montage Charity Ball,Barbra Hassan akiwakaribisha baadhi ya viongozi mbalimbali wa kiserikali,mabalozi na wageni waalikwa wengine waliofika kwenye hafla hiyo ndani ya hotel ya Serena jijini Dar.
Pichani juu ni wageni waalikwa kutoka makampuni mbalimbali wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo,ambapo mgeni rasmi alikuwa Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete.
Kalunde Band wakitumbuiza jukwaani
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Barnaba akipewa kampani na baadhi ya wanamuziki wenzake jukwaani,wakitumbuiza mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani),ndani ya hotel ya Serena jijini Dar.
Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti wakiongozwa na MKurugenzi wao Mtendani (wa tatu kulia),Steve Gannon wakiwa katika picha ya pamoja,aidha kampuni hiyo pamoja na kudhamini hafla hiyo pia ilichangia kiasi cha shilingi milioni tano
Baadhi ya magauni yakinadiwa kwa staili ya kipekee kabisa,kwa ajili ya kuchangia mfuko huo wa kuwasiadia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball.
PICHA ZOTE NA Michuzijr.
Comments