MILOVAN ATUA DAR MASHABIKI WA SIMBA WAMBEBA

DAR ES SALAAM, Tanzania

HATIMAYE aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba Mserbia Milovan Cirkovic, ameamua kutua nchini ili kuhakikisha Uongozi wa klabu hiyo unamlipa madai yake yaliyosalia mara baada ya kuvunja nae Mkataba.

Milovan amesema, ameamaamua kuja nchini kudai stahiki zake mara baada ya kuona uongozi ukishindwa kulitatua suala hilo.
Alisema amekuja na hatoondoka mpaka atakapoakikisha analipwa fmadai yake ambayo anayadai na kudai kushangazwa na viongozi kushindwa kupokea simu zake anapowapigia.

Milovan amefikia katika juzi Hoteli ya Spice jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwaona viongozi wa Simba ili apate haki yake na kurudi kwao Serbia.

Kocha huyu alitupiwa vilago kwa madai ya timu yake kutofanya vizuri katika baadhi ya mechi zake mwishoni mwa raundi ya kwanza na nafasi yake kutwaliwa na Mfaransa Patric Lieweg.

Katika hatua nyingine mashabiki wa Simba waliohudhuria pambano la kimataifa kati ya Stars na Cameroon walimbeba juju kocha huyo mara baada ya kumalizika kwa pambano hilo huku wakiimba 'huyu ndiye kocha wetu huyu ndiye kocha wetu' babu hatumtambui.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.