Nigeria 2 Ivory Coast 1
Kipindi cha pili kinaelekea ukingoni. Nigeria 2 Ivory Coast 1.
Nigeria ndiyo iliyokuwa ikiongoza kwa kufunga
bao kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji wake Emmanuel Emenike katika
dakika ya 45.Ivory Coast ilisawazisha bao hilo baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Didier Drogba na kumfikia mfungaji Cheick Tiote katika dakika ya 51 na kuunganisjha kwa kichwa mpira huo.
Kikosi cha Ivory Coast ambacho kilionekana kuwa ni bora zaidi katika michuano hii, kimeonekana kuendelea na mkosi wake kama ilivyokuwa mwaka jana wakitolewa katika fainali na Zambia, timu ambayo haikupewa nafasi.
Hata hivyo timu zote zinazidi kushambuliana kwa sababu kufungwa kuna maana ya kuyaaga mashindano haya ya mwaka 2013.
Comments