TAARIFA KUTOKA CHAMACHA MAPINDUZI CCM

                           TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi itafanya Mkutano wake wa kawaida kuanzia tarehe 10 -11 /02/2013. Kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.


Wajumbe wa NEC wanatarajiwa kufika Mjini Dodoma leo tarehe 9/02/2013,kwa ajili ya kikao hicho.


Pamoja na mambo mengine kikao hichi kitatanguliwa na Semina ya siku mbili kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.


Lengo la Semina hii ni kuwaongezea Wajumbe uelewa kuhusu masuala ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake hasa ikizingatiwa kwamba wengi wa Wajumbe ni wapya kufuatia Uchaguzi Mkuu wa CCM wa mwaka 2012.


Mada zitakazowasilishwa kwenye Semina ni pamoja na;

1. Nafasi na Wajibu wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa

2. Umuhimu wa Maadili kwa Viongozi na Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi.


3. Mikakati ya kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa nane wa CCM.


4. Mkakati wa kukuza ajira nchini.


Semina hii itafuatiwa na Mkutano rasmi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ambao pamoja na mambo mengine utafanya Uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi.


Imetolewa:​
Nape Moses Nnauye
KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZ

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.