*WAKAZI WA MKOA WA LINDI WATAKIWA KULIMA ZAO LA MTAMA ILI KUKABILIANA NA NJAA


Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete akikagua bidhaa za wajasiriamali, alipotembelea eneo la Raha Leo, Lindi mjini leo Februari 17, 2013. akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa chama mkoani Lindi.
Mkazi wa Raha Leo, akiuliza swali kwenye mkutano huo.picha na Bashir Nkolomo
*******************************************************
Na Anna Nkinda – Maelezo , Lindi
Wakazi wa mkoa wa Lindi wametakiwa kurudia kulima kwa wingi zao lao la asili la chakula la mtama kwani zao hilo linastahimili hali ya ukame na hivyo kuweza kukabiliana na janga la njaa linaloukabili mkoa huo mara kwa mara.
Wito huo umetolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa (NEC) Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwa nyakati tofauti na wananchi wa kata za Tandangongoro, Ng’apa na Rahaleo  zilizopo katika wilaya ya Lindi mjini wakati wa ziara yake ya kichama ya siku saba wilayani humo.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais alisema kuwa hali ya hewa ya mkoa wa Lindi ni ya ukame na kipindi cha  miaka ya nyuma wakazi wa mkoa huo walikuwa wanalima kwa wingi zao la mtama lakini hivi sasa baadhi yao wameacha kulima zao hilo na  kulima mpunga ambao haustahimili ukame na hivyo kukabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula.
“Licha ya kulima  kilimo cha kisasa cha  zao la mtama, pia mnaweza kulima zao la muhogo ambalo ndani ya hekari moja unavuna  magunia 20 ambayo ni sawa na tani 2 ambazo unaweza kuuza na zingine  kula pia mlime mazao ya biashara kama korosho na ufuta ambayo yatawasaidia kupata kuinua kipato”, alisema Mama Kikwete.
Aidha Mjumbe huyo wa NEC pia aliwataka wanawake kutokuogopa na kuona aibu  kuuliza maswali kwa viongozi wa Serikali na vyama vya siasa wakati wa mikutano ya hadhara kwani kwa kufanya hivyo kutawasaidia  viongozi wao kujua kero zinazowakabili  na kuweza kuwasaidia.
Mama Kikwete alihoji, “Tumieni haki yenu ya msingi kwa  kuuliza maswali kwani wanawake wengi na watoto wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa huduma bora ya afya , sasa kama mtanyamaza kimya mnadhani viongozi watajua kero zinazowakabili”?.
Kwa upande wake Meya wa Lindi Mjini Frank Magali alisema kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa chakula wa tani 287 ambazo waliomba msaada Serikalini na kufanikiwa kupewa  tani 172.2 za mahindi kati ya hizo tani 17.2 watazigawa bure kwawatu wasiojiweza na tani 155 zitauzwa kwa wananchi kwa shilingi 50 kwa kilo moja.
“Hadi sasa hakuna mwananchi yeyote aliyepoteza maisha kwa ajili ya njaa lakini kata zote 18 za wilaya hii zinaupungufu wa chakula  lakini ukubwa wa tatizo unatofautina  na kata iliyoathirika zaidi ni ya Mtanda ambayo itapata msaada wa tani 58 za mahindi”, alisema Magali.
Katika mikutano hiyo jumla ya wanachama  wa CCM  46, Umoja wa vijana 51, Umoja wa Wanawake  79 na Jumuia ya Wazazi  105 walijiunga na chama hicho pia  wananchi walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na kero zinazowakabili yakiwemo masuala ya afya, elimu, umeme, barabara na ma

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI