*YANGA NA AFRICAN LYON ZAINGIZA SH.M.68/=


Mechi namba 119 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Februari 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kuibuka ushindi wa mabao 4-0 imeingiza sh. milioni 68,438,000. 

Watazamaji 12,147 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 16,170,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,439,694.92. 

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo 10,982 walikata tiketi hizo na kuingiza sh. 54,910,000. 

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 8,222,162.26, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,933,297.36, Kamati ya Ligi sh. 

4,933,297.36, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,466,648.68 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam(DRFA) sh. 1,918,504.53.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.