Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto) na Mwakilishi wa JICA nchini Yasunori Onishi  (kulia) wakibadilishana hati za mkataba wa Japan kusaidia shilingi bilioni 1.28 kwa ajili ya usambazaji wa maji safi na salama katika baadhi ya vijijini vya mkoa wa Tabora.
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) wakibadilishana hati za mkataba wa Japan kusaidia shilingi bilioni 1.28 kwa ajili ya usambazaji wa maji safi na salama katika baadhi ya vijijini vya mkoa wa Tabora.
---
Serikali ya Japan kupitia Shirika la JICA imesaini mkataba  wa kuisaidia Tanzania  shilingi Bilioni 1.28 za kusaidia usambazaji maji katika mkoa wa Tabora .
 Fedha hizo zimetolewa leo(jana) na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mh. MASAKI OKADA katika sherehe iliyofanyika jijini Dar es salaam.
 Akipokea msaada huo kwa niaba ya Tanzania Waziri wa Fedha Mh. Dkt. William Mgimwa alisema msaada huo utasaidia kupunguza kero ya upatikanaji wa maji katika baadhi ya vijiji mkoani Tabora na pia kukabiliana na vita dhidi ya umaskini.
 ‘’Ninafurahi ya kuona kwamba makubaliano ya msaada huu tulio saini hivi punde utaiwezesha serikali yako ya Japan kupitia kampuni ya JICA kutupatia fedha za Kijapan Yeni 76 milioni sawa na shilingi bilioni 1.28 za kitanzania, kwaajili ya kusaidia utekelezaji wa usamabazaji maji vijijini katika mkoa wa Tabora”. Mh. Dkt, Mgimwa alisema.
 Aidha Dkt Mgimwa kwa niaba ya Serikali ya Jamuhuri ya Tanzania aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaada wake huo  muhimu ambao umekuja  muda muafaka wakati Tanzania iko katika mapambano dhidi ya umaskini ikiwemo kuhakikisha wanapata maji safi na salama.
 Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Tanzania Mh, MASAKI OKADA alisema kuwa  Japan tangu mwaka  1996,inatekeleza miradi sita ya maji katika mikoa ya Kagera ,Singida, Manyara , Shinyanga ,Mwanza , Mara, Mtwara , Lindi, Pwani , Dar es Salaam pamoja na Zanzibar.Alisema kuwa hadi hivi sasa jumla ya watu laki nane na sitini elfu wamenufaika na miradi hiyo hapa  nchini Tanzania.
 Japan na Tanzania zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu ambapo hadi hivi sasa uhusiano wa Nchi hizo umedumu kwa muda wa miaka 50
Na
 Benedict Liwenga
Idaya ya Habari Maelezo-Dar es Salaam

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI