HAYA NI MAUZA UZA YA KARNE IRINGA , MJANE AKIMBIA NYUMBA KWA MAUZA UZA YA MOTO KUWAKA MARA KWA MARA

Mali mbali mbali  zilizoteketea na kutupwa hapa zikiwa mkaa
Mwenyekiti  wa serikali ya mtaa wa Beila Kata ya Kwakilosa mjini Iringa Alen Koma koma akionyesha madaftari ya  mwanafunzi mtoto  wa mjane huyo aliyekimbia nyumba baada ya  kuonekana kimiujiza leo baada ya kupotea toka jana
Diwani  wa kata  hiyo ya Kwakilosa  Hamza Ginga  akiwa ameshika mkoba  wa mjane huyo uliopotea pamoja na madaftari ya  watoto  kimiujiza
Hiki ni kitanda kilichoungua kimiujiza na moto  huo
Hili ni paa la nyumba  hiyo inayoungua kimiujiza kwa zaidi ya mara  tano  sasa kama inavyoonekana ikiwa  salama salimini 
 


Mwanamke  Bi. Faraja  Chengula (31) na  watoto  wake  akiwa na familia yake pamoja na diwani  wa kata ya Kwakilosa mheshimiwa Hamza Ginga na baadhi ya  viongozi  wa mtaa huo wa Beila  baada ya mali katika  nyumba yake  kuteketea kwa moto wa miujiza .



Majane Bi Faraja Chengula 
........................................... 
HUJAFA  hujaumbika bado ni kauli ya mwanamke  mkazi  wa mtaa wa  Beila kata ya Kwakilosa katika  Manispaa ya  Iringa Bi. Faraja Chengula (31) ambae amelazimika  kuikimbia  nyumba aliyopanga  na kwenda  kuomba hifadhi kwa kiongozi mmoja  wa  kidini kama njia ya  kujinusuru na mauza uza haya moto  kimiujiza umeendelea  kumtesa kwa kuteketeza  mali mbali mbali  bila  kuleta madhara kwa  binadamu.
Akizungumza na mtandao huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com  leo mwanamke  huyo ambae  ni mjane  aliyepoteza mwenzi  wake kwa zaidi ya miaka  mitatu  sasa  alisema  kuwa mauza uza hayo ndani ya  chumba chake yalianza  toka jumatano ya April 17 mwaka  huu baada ya  kurejea  nyumbani  na kupatwa na  wakati mgumu  kutafuta  ufunguo wa nyumba ambao ulipotea katika mazingira  tata.
Bi. Chengula  alisema  kuwa mbali ya kupotea ufunguo huo  bado  aliendelea  kushuhudia mauza uza mbali mbali  ikiwa ni pamoja na kuibuka kwa moto ambao chanzo chake bado kufahamika na mbaya  zaidi moto huo ulikuwa unawake katika kitanda  bila  kuteketeza  godoro na baada ya kuuzima kwa maji bado uliibuka  moto mwingine katika  mito ya makochi aliyokuwa ameiweka nje ya  chumba  hiyo.
“ Kweli nashindwa  kuelezea  ila nilishangazwa  zaidi  baada ya kuona mito  hiyo ya makochi  iliyokuwa  nje ya  chumba ghafla  ikiwa ndani ya  chumba na kuwaka  moto huku  nikishuhudia moto  huo  ukishika kasi na hata nilipojaribu  kuzima kwa maji  ilishindikana “
Hata  hivyo  alisema  kuwa hadi  sasa bado hajatambua  miujiza  hiyo  inatokana na  nini kwani toka  mume   wake amefariki  dunia  ni  zaidi ya miaka  miwili  sasa na hakuna jambo lolote kama  hilo ambalo  limepata  kujitokeza na kuwa  mbaya  zaidi  mazingira ya  moto  huo yamekuwa  wakimshangaza  kila mkazi wa nyumba hiyo  yenye wapangaji  zaidi ya 10 pamoja na majirani  wanaozunguka nyumba  hiyo.
Bi.Chengula  alisema  kuwa wakati  mwingine  amekuwa akizikuta nguo  zake na  za  watoto  wake  wawili  chooni na baada ya  kurejea ndani ya  chumba  hicho amekuwa akizikuta  zikiwa ndani na mara nyingine moto huo  umekuwa  ukiwaka katika eneo la  sokte  ya umeme bila  sokte  hiyo ya plastick kuguswa na moto  huo .
“Kweli nashindwa  kujua chanzo cha mambo haya kwa  sijala kituo cha mtu yeyote na mimi ni mlokole ninayesali kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Mlandege na mbali ya kufanya maombi kanisani  ila bado mambo haya  yameendelea  kuniandama na  zaidi ya mara  tano  sasa moto  unawake ndani ya  chumba  changu  pekee “
Aidha  alisema  kutokana na mauza uza hayo kuchukua kasi alilazimika  kuwaita waumini  wenzake na kufanya maombi katika  chumba  hicho ila  wakati  wakiendelea kufanya maombi ghafla  walijikuta  simu  za viganjani  zikiwa  zimepotea katika mazingira yenye utata na hadi  sasa  simu  hizo  hazijapatikana.
Pia  alisema  kuwa juzi  katika mazingira tata  madaftari ya  wanafunzi  yaliyokuwa katika mfuko ,mkoba  wake  wa mkononi  uliokuwa na vitu  mbali mbali  pamoja na pea  moja ya  viatu  vyake  vilipotea katika mazingira  tata ila  leo April 26 majiar ya saa 2 asubuhi  baada ya  viongozi  wa  serikali ya mtaa na diwani  kufika eneo hilo wakiwa na mwandishi  wa habari hizi vitu hivyo  vilionekana eneo ambalo ni jeupe  sana pamoja na kuwepo kwa umande katika  eneo hilo ila vitu  hivyo havikugusa hata tone la umande.
Balozi  wa mtaa huo  wa Beila Bi. Christina Ndale  alisema kuwa  nyumba  hiyo ambayo imekuwa  ikiandamwa na mauza uza hayo ni nyumba Block ‘Y’ 79 na  kuwa wao kama  mtaa wamepata  kushuhudia mauza uza hayo nab ado  wanaumiza  vichwa  kujua  chanzo cha mambo hayo .
 Wakati mwenyekiti  wa  mtaa huyo Alan Koma koma  alisema  kuwa mauza uza kama hayo  si mara ya kwanza  kujitokeza katika mtaa huo kwani kwa  upande wake  pia mambo kama hayo yalipata kumtokea kwa nyumba yake kupigwa mawe  usiku kucha na  watu  wasiofahamika  mbali ya  kulindwa na askari  polisi  na  wananchi  kuzunguka nyumba  hiyo kwa ulinzi  wa sungusungu ila bado mawe hayo ambayo  yalikuwa  yakimwagika kama mvua  kutoka angani yaliendelea  kushambulia nyumba hiyo .
Hivyo  alisema suala  hilo la mauza uza  ni miongoni mwa mambo ambayo yanawatesa  wakazi  wa eneo hilo hivyo  kuwaomba  watu  wanaojihusisha na imani  za kishirikina kwa ajili ya kuwatesa wengine  kuachana na masuala  hayo.
Diwani  wa kata ya Kwakilossa mheshimiwa  Hamza  Ginga akithibitisha  kutokea kwa matukio hayo alisema  kuwa yeye kama  diwani anashindwa  kujua  sababu  kuu ya mambo hayo japo ana mpango  wa kuitisha mkutano  ili kukutana na  wananchi wake  wote kama njia ya  kumaliza mauza uza hayo.
Mheshimiwa Ginga  alisema kwa sasa wanakusudia  kuwaita  viongozi  wa dini   waliopo mjini Iringa  kutoka nchini Kenya , Uganda na mwenyeji  wao askofu  wa kituo cha maombezi na uponyaji cha Overcomers Power Center Dkt  Boaz Sollo ali kufanya maombi maalum katika nyumba  hiyo na kumtaka mwamake huyo kutoukimbia mtaa kutokana na mauza uza hayo kwani hata kama atahama kama kuna mtu anamfuatilia ataendelea  kufanya hivyo.
MWISHO

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.