- Get link
- Other Apps
HUKUMU YA PONDA YAAHIRISHWA HADI MEI 9
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda (kulia) akiwa na mshtakiwa
mwenzake Saleh Mkadamu wakielekea kupanda basi la magereza baada ya
hukumu ya kesi yao ya uchochezi kuahirishwa hadi Mei 9. Sheikh Ponda
Issa Ponda na wenzake 49 wanakabiriwa na makosa matano ya kula njama na
kuingia kwa jinai katika uwanja namba 311/3/4 kitalu T uliopo Markaz
Chang'ombe na wizi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya Shs
milioni 59 mali ya kampuni ya Agritanza.
Saleh Mkadamu akipanda basi kuelekea mahabusu
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda akipanda basi la magereza.
Ulinzi mkali kila kona ya mahakama
Askari wakiimarisha ulinzi nje ya Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Msafara wa magari ya Polisi
wakisindikiza gari la magereza lililomchukua Katibu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda wakati wakielekea
mahabusu baada ya hukumu ya kesi yao kuahirishwa leo hadi Mei 9.
Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa
wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam leo wakati hukumu ya kesi yake ilipoahirishwa leo.Picha na Habari
Mseto Blog
Comments