MAMBO YA PASAKA , JEMBA AZIMA BAADA YA KUGUGUMIA POMBE YA OFA AKIJIANDAA NA PASAKA

 Meneja wa Club ya V.I.P mjini Iringa Mick akiwa  amezima baada ya kunya viroba na kisichana kwa  kuonyesha uwezo  wake na baada ya dakika 20 akazima kama hivi ,hapa nalazimika  kukumbuka ule ujumbe wa  chonde chonde! ulevi Nomaaaaaaaaaa!?
 Hii ni karibu Pasaka kweheri ijumaa kuu
 Mlinzi  wa eneo la TFA akijaribu kumsaidia baada ya polisi kufika na kuamua kumwacha kutokana na ugonjwa wake wa pombe kutokuwa na daktari wa kutibu
 
 Wasamaria  wema   wakimtazama meneja huyo chapombe akiwa amezima
 ....................................................................................
Ukisema ulevi noma wapo watakaosema ulevi ni sehemu ya kupoteza mawazo ila kwa tukio hilo kila mmoja anaweza ungana nami kuwa kweli ulevi noma hapa ni eneo na TFA mjini Iringa ambapo hadi sasa meneja  huyu wa Club ya V.I.P akiwa amezima kwa kunywa pombe kupita  kiasi 

Wakati  sikuu ya Pasaka  inafikia  ukingoni  leo kwa  waumini  wa dini ya  Kikristo ulimwenguni  kusherekea  siku hiyo ya  kumbukumbu ya kufufuka kwa  Yesu Kristo ,katika mji  wa Iringa mbali ya  idadi kubwa ya  wananchi kula pasaka kwa hali ya utulivu  na amani  ila  baadhi yao  wameamkia Hospitali baada ya  kunywa  pombe  kupita kiasi .

katika  tukio  lililotokea katika eneo moja maarufu mjini Iringa ni baada ya  kijana anayesadikika kuwa ni meneja  wa Club V.I.P Bw Mick kuonyesha ujanja  wake katika kunywa  pombe kali aina ya konyagi na kupelekea  kupoteza fahamu na kulazwa katika  Hospitali ya  Rufaa ya mkoa  wa Iringa akitibiwa ulevi wa  pombe  kupita  kiasi.

Tukio hili si tu  linashangaza  ila linasikitisha  japo pia ni fundisho kwa wengine  wenye tabia ya  kunywa  pombe  kupita  kiasi kama  hivi.

Kijana  huyo anadaiwa kuwa na tabia ya kuomba omba  pombe kwa  watu pindi anapotembelea  bara mbali mbali na  siku  hiyo ya mkesha  wa  pasaka wale  waliochoka  kuombwa ombwa pombe  waliamua  kuchanga  pesa na  kumpa ofa ya  pombe kiasi cha kumfanya kijana  huyo  kujigamba kuwa ana weza kunywa konyagi chupa ndogo (Visichana) hata  vitano kwa mpigo jambo ambalo alilianza kwa kunywa chupa mbili na viroba 5 na baada ya  dakika 15 alianguka na kupoteza fahamu kwa siku  mbili  sasa bado yupo hoi Hospitali .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.