RONALDO AIPELEKA REAL NUSU FAINALI ULAYA, ILA DROGBA, SNEIJDER BADO MOTO
WABABE wa Hispania, Real Madrid wamefuzu
kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya jana usiku
kufungwa 3-2 Galatasaray nchini Uturuki katika mchezo wa marudiano wa
Robo Fainali.
Kwa matokeo hayo, kikosi cha Jose
Mourinho kimesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-2, baada awali
kushinda 3-0 katika mchezo wa kwanza nchini Hispania.
Jana Cristiano Ronaldo alikuwa wa kwanza kufunga bao dakika ya saba, lakini Emmanuel Eboue akaisawazishia Gala dakika ya 57, kabla Wesley Sneijder hajawafungia wenyeji bao la pili dakika ya 70.
Utu uzima dawa: Didier Drogba alikuwa mmoja wa wafungaji wa mabao ya Galatasaray jana
Dakika mbili baadaye, Did Drogba
akafunga bao la tatu, kabla ya Ronaldo kufunga tena dakika ya 90 na
kuiweka sawa barabarani Real katika mbio zake za kukimbilia taji la 10
Ulaya.
Katika mchezo huo, kikosi cha Galatasaray kilikuwa: Muslera,
Eboue/Elmander dk80, Zan, Kaya, Riera, Altintop/Amrabat dk46, Felipe
Melo, Inan, Sneijder, Bulut /Sarioglu dk63 na Drogba.
Real Madrid: Diego
Lopez, Essien/Arbeloa dk31, Pepe, Varane, Fabio Coentrao, Khedira,
Modric, Di Maria, Ozil/ Albiol dk81, Ronaldo na Higuain/Benzema dk73.
Shangwe za bao: Drogba akishangilia baada ya kufunga bao la tatu
Ronaldo akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza
Drogba akimpongeza ndugu yake, Emmanuel Eboue kuisawazishia Gala jana
Wesley Sneijder akishangilia bao lake
Ronaldo akishangilia bao lake la pili jana
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho akipeana mikono na kocha wa Gala, Fatih Terim baada ya mechi
Katika mchezo mwingine jana, Borussia
Dortmund ilifanikiwa kushinda 3-0 dhidi ya Malaga kwenye Uwanja wa
Signal Iduna Park, hivyo kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-2, baada ya
awali kufungwa 2-0 Hispania.
Comments