Tanzania haitarudi nyuma kwenye kuingilia kati DRC

Na Deodatus Balile, Dar es Salaam

Dar es Salaam haitarudi nyuma katika kupeleka majeshi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kama sehemu ya kikosi cha kuingilia kati cha Umoja wa Mataifa, licha ya maonyo mawili ya maandishi kutoka kikundi cha waasi cha March 23rd Movement (M23), maafisa wa Tanzania wasema.
  • Waasi wa M23 wakiondoka toka milimani tarehe 30 Novemba, 2012, baada ya kuondoka kijiji cha Karuba cha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. [Na Phil Moore/AFP] Waasi wa M23 wakiondoka toka milimani tarehe 30 Novemba, 2012, baada ya kuondoka kijiji cha Karuba cha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. [Na Phil Moore/AFP]
  • Mkuu wa kijeshi wa M23 Jenerali Sultani Makenga (katikati) akiwaashiria baadhi ya maafisa wake karibu na mji wa Sake, mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 30 Novemba, 2012. [Na Phil Moore/AFP] Mkuu wa kijeshi wa M23 Jenerali Sultani Makenga (katikati) akiwaashiria baadhi ya maafisa wake karibu na mji wa Sake, mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 30 Novemba, 2012. [Na Phil Moore/AFP]
Salva Rweyemamu, mkurugenzi wa mawasiliano wa raisi wa Tanzania, aliiambia Sabahi kuwa serikali ilipokea barua mbili kutoka kikundi cha M23, ambacho kinapigana ili kuiangusha serikali ya Kongo.
Barua ya kwanza ilielekezwa kwa Mwenyekiti Mkutano wa Kimataifa wa Maziwa Makuu, Raisi wa Uganda Yoweri Museveni, na nyakala kupelekwa kwa wakuu wote wa serikali wa kanda hiyo, akiwemo Raisi wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Barua ya pili ilitumwa kwa spika wa Bunge la Taifa Anne Makinda na kutiwa saini na Bertrand Bisimwa, mkuu mpya wa tawi la kisiasa la M23, iliyofika bunge la Tanzania siku ya Jumamosi (tarehe 20 Aprili), vyanzo viliiambia Sabahi.
Katika barua hiyo, M23 iliwataka wabunge wa Dar es Salaam kuishauri serikali dhidi ya kupeleka majeshi huko DRC, na hata kutishia "mauaji" ya majeshi ya Tanzania na wapiganaji wa M23 ikiwa Tanzania itaendelea mbele na upelekaji wa majeshi yake huko.

Kurejesha amani

"Lengo la majeshi ya Tanzania sio kuwaua Wakongo bali kurejesha amani," naibu Spika wa Bunge la Taifa la Tanzania Job Ndugai aliiambia Sabahi. "M23 wataona hili kuwa ni tatizo ikiwa hawataki amani. Hatupeleki askari wetu kwenda kuua au kuuliwa na M23."
Hapo tarehe 28 Machi, Baraza la Usalama la UN kwa kauli moja lilipitisha Azimio 2098, ambalo lilisafisha njia kwa chombo cha kwanza cha kimataifa cha kikosi cha "mashambulizi". Mamlaka ya kikosi hicho cha kuingilia kati, itakayoundwa na vikosi vya askari wa miguu kutoka Tanzania, Afrika Kusini, Msumbiji na Malawi, ni "kuwamalizia nguvu na kuwanyang'anya silaha" wa M23, waasi wa Kongo na vikundi vyenye silaha vya kigeni huko mashariki ya DRC, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Umoja wa Mataifa.
Katika barua ya tarehe 11 Aprili, Bisimwa alionya kwamba M23 itaishinda kikundi cha UN itakachoongozwa na jenerali wa Tanzania.
Mnamo tarehe 7 Aprili, Bisimwa alitoa vikosi kama hivyo kwa majeshi ya Afrika Kusini katika akaunti yake ya Twitter, lakini Afrika Kusini ilisema kuwa itaendelea na mipango yake ya kujiunga na kikosi cha uingiliaji kati cha UN huko DRC.
Kwa majibu ya barua ya Bisimwa kwa Spika Makinda, Azimio 2098 "linabadilisha Misheni ya UN ya Kulinda Amani huko DRC na kuifanya kuwa kikosi cha vita chenye amri ya kufanya operesheni za mashambulizi dhidi ya wananchi wa Kongo".
Bisimwa, ambaye anaushutumu Umoja wa Mataifa kwa kuingilia kati DRC kwa ajili ya kuiokoa serikali ilioko madarakani, kiliapa kuwa vikosi vya M23 vitaishinda kikosi cha uingiliaji kati.
Alisema kuwa anamheshimu sana raisi wa kwanza wa Tanzania, marehemu Mwalimu Julius Nyerere, lakini bado M23 itakuwa haina chaguo jengine bali "kuyaua majeshi ya ndugu zao kutoka Tanzania".
Kanali Kapambala Mgawe, msemaji mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi la Tanzania, alirudia kusema kuwa vikosi vya Tanzania vinakwenda Mashariki mwa DRC kuleta amani katika eneo hilo.
"Ambapo maisha ya wananchi wa DRC au walinda amani itakuwa katika hali ya hatari, vikosi vyetu vitaokoa maisha na kuwanyang'anya silaha wale wanaosababisha hatari hiyo," aliiambia Sabahi. "Huu ni msimamo na maelekezo kutoka UN."

Vitisho huko nyuma

Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa Bernard Membe aliiambia Sabahi kuwa Tanzania imezowea kupokea vitisho kama hivyo visivyo na msingi kutoka vikundi vya waasi kila mara majeshi yake yanapoingilia kati kuwaokoa watu wasio na hatia.
Kama mfano, alitaja uingiliaji kati kijeshi wa Umoja wa Afrika huko Anjuan, katika visiwa vya Komoro, ambao ulimuondoa madarakani raisi wa zamani Kanali Mohamed Bacar. Licha ya vitisho kama hivyo dhidi ya mchango wa majeshi kutoka Dar es Salaam, vikosi vya Tanzania havikurudi nyuma, Membe alisema.
"Nadhani wao [M23] wangemuenzi Mwalimu Nyerere kwa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vinasababisha ubakaji uliotapakaa, vifo vya watoto na wanawake, na watu wanaokimbia makazi yao," alisema.
Membe alisema M23 kinapaswa kumaliza uasi wake na kuacha kuua watu wasio na hatia, kwa hivyo kutoipa Tanzania sababu yoyote ya kupeleka kikosi chake DRC.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.