BARNABA, KIDUMU KUPAMBA MATEMBEZI YA HISANI 'STEP AHEAD WALK 2013

Msanii machachari wa Bongo Flava, Barnaba, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Matembezi ya Hisani ya 'Step Ahead Walk 2013,' yatakayopambwa na kibao chake kiitwacho Wanawake alichoimba kwa ushirikiano na Mrundi anayefanyia shughuli za muziki nchini Kenya, Jean Pierre Nimbona 'Kidumu.'
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano wa Barclays, Tunu Kavishe, akizungumza na waandishi wa habari (hawao pichani), wakati wa uzinduzi wa Matembezi ya Hisani ya Step Ahead Walk 2013 yatakayosindikizwa na Barnaba na Kidumu.


DAR ES SALAAM, Tanzania

'Step Ahead Walk’ ni mkakati endelevu wa Benki ya Barclays, ambao kusudi lake ni kujenga uelewa wa kusaidia mahitaji muhimu katika jamii. Matembezi hayo ya kila mwaka, yalizinduliwa mwaka 2008 hapa nchini na kusaidia kuelimisha jamii kuhusu uchangishaji fedha ili kusaidia masuala ya uzazi na afya ya watoto

KIBAO cha ‘Wanawake,’ kilichoimbwa na nyota Bongo Flava Barnabas Elias, akishirikiana na Mrundi Jean Pierre Nimbona ‘Kidumu,’ kimezinduliwa rasmi leo na kutangazwa kupamba Matembezi ya Hisani ya ‘Step Ahead Walk 2013,’ yanayoratibiwa na Benki ya Barclays Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano wa Barclays, Tunu Kavishe, alisema maudhui ya wimbo huo ni kuhamasisha wadau kujitokeza kwa wingi kushiriki ‘Step Ahead Walk’ ambayo lengo lake ni kuchangisha pesa kwa ajili ya kinamama na watoto wachanga.

Aliongeza kuwa, tukio hilo litafanyika Juni 8, 2013, katika hoteli ya Golden Tulip, likihusisha matembezi ya hisani ya kilomita tano, ambapo kila mtu katika jamii anakaribishwa kushiriki kwa kununua tiketi kwa silingi za Kitanzania 5,000 ambazo zinapatika katika matawi ya Benki ya Barclays kuanzia Aprili 29.

“Mwaka 2011, Benki ya Barclays na washiriki wake walifanikiwa kukusanya shilingi mil. 150 kutokana na mauzo ya tiketi na matoleo mengine kutoka kwa wafadhili, lakini mwaka huu lengo ni kuchangisha mara mbili ya kiasi hicho kutoka kwenye matoleo ya washirika muhimu na washiriki wengine katika jamii,” alisema Kavishe.

Alibainisha kuwa, kiasi kitakachochangishwa mwaka huu kitakwenda kusaidia katika masuala ya uzazi na afya ya watoto, ikiwamo Mafunzo kwa wakunga wa uzazi, matibabu ya Fistula na upasuaji kwa watoto waliozaliwa na ulemavu unaosababishwa na uzazi.

‘Step Ahead Walk’ ni mkakati endelevu wa Benki ya Barclays, ambao kusudi lake ni kujenga uelewa wa kusaidia mahitaji muhimu katika jamii. Matembezi hayo ya kila mwaka, yalizinduliwa mwaka 2008 hapa nchini na kusaidia kuelimisha jamii kuhusu uchangishaji fedha ili kusaidia masuala ya uzazi na afya ya watoto.

Kavishe alisisitiza kuwa, ‘Step Ahead Walk 2013’ itafanikiwa, kama tu itawezeshwa na kila mshiriki na jamii nzima ya Kitanzania, kwa hiyo akawataka wadau kujiunga katika matembezi hayo ili kuweza kuleta mabadiliko katika masuala ya afya ya Uzazi na Mtoto kwa ujumla hapa Tanzania.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.