BREAKING NEWS.....IRINGA NI SHWARI MACHINGA WAPINGA KUTUMIKA KISIASA ,RC IRINGA AWAPONGEZA MACHINGA KWA KUREJEA MLANDEGE

 Baadhi  ya maduka  eneo la Mashine  tatu mjini Iringa yakiwa  yamefungwa kwa  hofu ya kutokea  vurugu ,ambazo  hata hivyo hazijatokea baada ya machinga  kugoma  kutumiwa  kisiasa
 Hali  ilivyo eneo la Mashine tatu mjini Iringa
 Haya  ni maadishi  yanayosomeka HATARI yaliyochorwa na watu  wasiojulikana  usiku wa kuamkia jana kama sehemu ya  kuwatisha  wananchi na  kuhamasisha  vurugu kabla ya  jeshi la polisi kuweka  ulinzi mkali eneo hilo
 Wafanyabiashara  wa maduka   ya mchele  eneo la mashine tatu  wakiendelea na biashara zao kwa utulivu zaidi  leo
 Hili ndilo eneo la mashine tatu kama  linavyoonekana mchana  huu baada ya machinga kukubali kuheshimu  sheria  ya mipango miji na kuachana na mvutano  usio na tija kwao
 Amani  na utulivu  warejea eneo la Mashine tatu mjini Iringa ,wananchi waendelea na shughuli zao kama kawaida leo ,machinga wakubali kutii  sheria
 Askari  wa FFU akiwa katika ulinzi eneo la mashine tatu leo ambapo hali imetulia zaidi
 Askari   wa FFU mjini Iringa akipita  eneo la mashine tatu ambako machinga  walipanga  kufanya biashara na vurugu  leo ila hali ya amani  imetawala  zaidi  eneo hilo
 Askari wa FFU  wakiwa kazini  leo  eneo la mashine tatu
 Ulinzi waimarishwa  eneo la mashine tatu ,machinga wakubali kufanya  biashara  eneo la Mlandege kama awali
 Hivi ndivyo  hali ilivyo eneo la mashine  tatu  leo ni amani na utulivu kwenda  mbele hakuna mabomu leo
 Leo ni amani  zaidi  Iringa hakuna  vurugu  zozote

Hali ya amani na utulivu  imerejea  mjini Iringa baada ya machinga  kukubali kuendelea na biashara  zao katika eneo la Mlandege ambalo uongozi  wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa  iliwatengea wamachinga  hao .
 Uchunguzi  uliofanywa na mtandao  huu  wa www.matukiodaima.com katika  eneo  hilo umeshuhudia kuwepo kwa amani  zaidi na  wafanyabiashara  waliokuwa  wamefunga maduka  yao kuhofia amani kuvurugika  wameonekana  wakifungua maduka  yao  huku machinga  ambao  walihamasishwa na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa  (Chadema)  kurejea  eneo hilo wakionyesha kupuuza ushauri huo wa mbunge na kuelekea Mlandege kama Manispaa ilivyowataka .

Baadhi ya machinga  wamesema  kuwa  suala  hilo  la machinga  kurudi  eneo hilo lipo  kisiasa  zaidi na kuwa kama  si mbunge  kuwahamasisha machinga hao kupitia mikutano  yake  hakuna machinga ambae angerejea eneo hilo  kwani  wengi  wao kuwepo Mlandege  walionyesha  kukubali .

Hata  hivyo machinga hao  wamesema  kuwa  hata  waliofanya  vurugu  wiki iliyopita  si machinga ni  wahuni  kutoka maeneo mbali ambali ambao  walifanya fujo hizo na kuwa machinga kama machinga hana nafasi ya  kufanya vurugu  zaidi ya kutafuta  pesa.
Pia  uchunguzi  unaonyesha  jeshi la  polisi mkoa  wa Iringa  kujipanga  vema kwa siku ya jana usiku na leo ikiwa ni pamoja na  kuwakamata  baadhi ya  watu ambao  walikuwa  wakitoa kauli za kichochezi katika  vijiwe mbali mbali .
Huku  askari  wa FFU kwa mara ya kwanza usiku  wa kuamkia leo  walionekana  wakiweka ulinzi mkali katika maeneo mbali mbali ya mji  likiwemo eneo la soko la Kihesa ,Mlandege, Mashine tatu na maeneo mengine mengi  hali iliyopelekea  vikundi vya vurugu  kutoweka ghafla mjini Iringa na wale  waliokuwa wamepanga  kuvuruga amani  kuamua  kusitisha mpango  huo.
Wakati  huo  huo mkuu  wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma  amewapongeza machinga  kwa kukubali  kurejea eneo la Mlandege ambalo uongozi  wa Manispaa ya  Iringa  ulikuwa umewapangia na kuwa  hekima iliyoonyeshwa na machinga  hao  inapaswa  kuigwa na makundi mengine ambayo yamekuwa yakichochewa kufanya vurugu kutokana na matatizo yao.
"Kweli napenda  kuwapongeza  sana machinga  wametumia busara   sana baada ya  kikao chao na mstahiki meya  wa Manispaa ya  Iringa kuhusu  kutafuta  suluhu lao  .....bila  shaka  wameonyesha  kumsikiliza na kumheshimu  vema meya na  mimi kama  mkuu  wa mkoa nawaahidi  kuwa  suala lao  litatafutiwa  uvumbuzi  wa kudumu nawaomba  wawe na subira na kuepuka  kutumiwa na wana siasa  katika  suala  lao"
MWISHO

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.