KITABU CHA SOKA LA TANZANIA CHATIKISA WADAU, MWAKALEBELA KUKISAMBAZA WIKI IJAO MIKOANI!!

181066_568992019785435_478320816_n
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Mtunzi wa kitabu cha kwanza kutokea Tanzania kinachozungumzia soka la Tanzania kiitwacho “SOKA LA TANZANIA”, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kitabu chake kimepokelewa vizuri na wadau wa soka hususani siku ya mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga mei 18 mwaka huu uwanja wa Taifa ambapo Simba walichezea kichapo cha mabao 2-0.
Mwakalebela ameimbia FULLSHANGWE kuwa kitabu hicho kwa sasa kimeshasambazwa jiji zima la Dar es salaam “Jiji la maji chumvi” na sasa wanaanza mipango ya kukisambaza mikoani.
“Kila kona ya Dar es salaam kitabu hiki kimefika madukani, sasa tunajiandaa kukipeleka katika mikoa mbalimbali ili wadau wapate kukisoma kwa kina na kujifunza mambo mengi kuhusu soka la Tanzania”. Alisema Mwakalebela.
Zoezi la kukisambaza mikoani linaweza kuanza mwanzoni mwa wiki ijayo na kila kitu kinakwenda sawa hivyo wapenda soka wakae mkao wa kula.
 Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Shirikisho la Kandanda nchini (TFF), na mdau mkubwa wa kandanda Fredrick Mwakalebela alisema kitabu hicho gharama yake ni shilingi elfu kumi tu (10,000.
Mwakalebela alisisitiza kuwa kila anayependa maandeleo ya soka la Tanzania ni nafasi yake kutafuta nakala ya kitabu hiki kwani ni muhimu sana kwa kweli.
 “Kitabu kinazungumzia soka la vijana, wanawake, mpango wa rais Dkt. Kikwete kuendeleza soka letu, masuala ya makomandoo wa uwanjani, matatizo mbalimbali ya soka la Tanzania na nini kifanyike, hayo ni miongoni mwa mambo mazuri yanayopataikana katika kitabu hiki”. Alisema Mwakalebela.
Pia alisema amepokea pongezi nyingi sana kutoka kwa wadau kitu ambacho anaamini kuwa watu wanakipenda kitabu na wataendelea kukipenda zaidi.
Pia kitabu hicho kimezungumzia ujio wa kocha Marcio Maximo, wadhamini, uhusiano kati ya waandishi wa habari na TFF na changamoto mbali mbali za mpira wa miguu Tanzania.
“Pia nimeelezea mambo niliyojifunza chini ya Rais Leodegar Tenga kwa kipindi cha miaka minne nikiwa TFF, matatizo niliyokutana nayo kutoka kwa makamandoo na kuniita mimi muimba kwaya wakati wa utambulisho wangu wa kwanza  Juni 15, 2006,”. alisema Mwakalebel

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.