MTOTO AUWAWA NA KUWAMBWA MTINI.

MAPIGANO baina ya Kabila la Wasonjo na kabila la Wamasai wa Loita kutoka nchini Kenya yanayoendelea katika Kata ya Samunge wilayani Ngorongoro mkoani Arusha yameonesha kiwango cha ukatili binadamu anachoweza kufikia, baada ya kupatikana kwa mifupa ya mtoto iliyewambwa mtini.
Taarifa kutoka eneo la mapigano linasema kwamba mtoto huyo ambaye mifupa yake ilikutwa alifahamika kwa jina la Njibula Philemon(14) kutoka katika eneo la Kis
angiro na inasemekana aliuawa na kisha kuwambwa juu ya mti kiasi cha miezi mitatu iliyopita.
Tukio hilo ni moja ya matukio mawili ya mauaji katika mapigano yanayoendelea. Akiongelea tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji cha Kisangiro , Timothy Thomas alidai kuwa mtoto huyo alipotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa katika shughuli za ufugaji yeye, ndugu yake na baba yake mzazi.
Timothy alidai kuwa wakati wakiwa katika shughuli zao za ufugaji baba yake mzazi alikwenda kutafuta chakula lakini aliporudi hakumuona tena hadi alipopatikana akiwa amewambwa kwenye mti mkubwa huku nyama zake zote zikiwa chini na kubaki mifupa.
“Mara zote tunapoona tatizo huwa tunatoa taarifa kwa Polisi lakini wakati mwingine wanadai kuwa sisi ni waongo hakuna matukio kama hayo hivyo basi tuliamua kuzika mifupa tuu ya kijana wetu pamoja na baadhi ya nyama za mwili wake, “ aliongeza Timothy.
Katika tukio jingine Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Samunge Jonas Gilobei alisema mauaji ya mtoto wa pili Kelvin Ndambiseya (8) yalifanyika Mei 10 mwaka huu eneo la mlima Ngaremishani Kitongoji cha Mijuti.
Alidai wakati kundi la Wamasai wanawavamia wafugaji hao waliokuwa wakubwa walikimbia kwa kuwa hawakuwa na silaha lakini mtoto huyo aliamua kujificha kwenye kundi kubwa la ng’ombe.
Aliendelea kufafanua kuwa wakati akiwa amejificha kwenye kundi hilo Wamasai waliweza kumuona mtoto yule na kumpiga risasi.
Alidai kuwa mara baada ya mtoto huyo kuuliwa katika mgogoro huo, wafugaji wengine waliokimbia katika eneo hilo walikuja kutoa taarifa kwa wanakijiji wengine ambao walilazimika kwenda kwenye eneo la tukio ambapo wale waliofika kwanza waliweza kuona mwili wa kijana huyo akiwa amekufa pamoja na mbwa wake.
Pia alisema kuwa mara baada ya hapo walijipanga na kuingia msituni kwa ajili ya kutafuta mwili huo ambapo hakupatikana hali ambayo inaongeza majonzi katika eneo hilo siku hadi siku.
Wakati huo huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alidai kuwa mpaka sasa ana taarifa juu ya kupotea kwa mtoto yatima Kelvin Nambiseya lakini bado hana taarifa juu ya kifo chake wala mtoto aliyewambwa juu ya mti kwa miezi 3.
You might also like:

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.