Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba afungua Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, jijini Dar es Salaam, aitaka Serikali kuiomba radhi Saud Arabia

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akiteta jambo na Katibu wake Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, kabla ya kukifungua kikao cha siku mbili cha  Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, Makao Makuu, Buguruni Dar es Salaam leo, Mei 14, 2013. (Picha zote na Kassim Mbarouk-bayana.blogspot)
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika kikao hicho kabla ya kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wake, Machano Khamis Ali, ili kumkaribisha Mwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Zanzibar Hamad Masoud Hamad.
Makamu Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali, akizungumza wakati alipokuwa akimkaribisha Mwenyekiti wake Profesa Ibrahim Lipumba (katikati) kwa ajili ya kuzungumza. Kulia ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad. 
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Kuu la Uongozi la chama hicho, wakati alipokuwa akikifungua kikao chao cha siku mbili, Makao Makuu, Buguruni Dar es Salaam leo. Pamoja na mambo mengine Lipumba, alizungumzia masuala mbalimbali yaliyojitokeza nchini hivi karibuni, ikiwemo migogoro ya tofauti za kidini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wake, Machano Khamis Ali na kulia Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza katika kikao hicho cha Baraza la Kuu la Uongozi la chama hicho, wakati alipokuwa akikifungua kikao, Makao Makuu, Buguruni Dar es Salaam leo. Pamoja na mambo mengine Lipumba, alizungumzia masuala mbalimbali yaliyojitokeza nchini hivi karibuni, ikiwemo migogoro ya tofauti za kidini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa, Machano Khamis Ali, Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad (wa pili kulia) na Naibu wake, Hamad Masoud Hamad.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza katika kikao hicho cha Baraza la Kuu la Uongozi la chama hicho, wakati alipokuwa akikifungua, Makao Makuu, Buguruni Dar es Salaam leo. 
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa kazini, wakati Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alipokuwa akizungumza wakati akikifungua kikao cha Baraza la Kuu la Uongozi la chama hicho, Makao Makuu, Buguruni Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo, la Uongozi la CUF, wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba wakati akikifungua kikao chao cha siku mbili, ukumbi wa Shaabani Khamis Mloo, Makao Makuu ya chama hicho, Buguruni leo. 
Baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo, la Uongozi la CUF, wakiwa katika kikao chao hicho, wakimsikiliza Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba wakati alipokuwa akihutubia wakati anakifungua kikao hicho cha siku mbili, ukumbi wa Shaabani Khamis Mloo, Makao Makuu ya chama hicho, Buguruni leo. 

Baadhi ya waandishi wa habari, wakiandika habari wakati Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akikifungua kikao cha Baraza Kuu, Makao Makuu, Buguruni Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akisisitiza jambo, wakati alipokuwa akikifungua kikao cha Baraza la Kuu la Uongozi la chama hicho, Makao Makuu, Buguruni Dar es Salaam leo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa, Machano Khamis Ali na kulia Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo, la Uongozi la CUF, wakifuatilia na kunakili hotuba ya Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba wakati akikifungua kikao chao cha siku mbili, ukumbi wa Shaabani Khamis Mloo, Makao Makuu ya chama hicho, Buguruni leo. 

Na Neema Mgonja
SERIKALI imetakiwa kuiomba radhi nchi ya Saud Arabia, kwa kitendo chake cha kuwakamata na kuwaachia huru raia watatu wa nchi hiyo, kwa tuhuma za kuhusika na tukio la mlipuko wa bomu lilotokea mkoani Arusha hivi karibuni.

Kauli hiyo, ilitolewa leo, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa Baraza Kuu la chama hicho.

Prof. Lipumba alisema kuwa kitendo cha raia hao, wa kigeni kukamatwa na kuhusishwa na tukio hilo, kisha kuachiwa kwa kukosekana ushahidi wa uhusika wao, kinapaswa kuikumbusha Serikali kuiomba radhi nchi hiyo, ili kudumisha ushirikiano.

Alisema kila aliyepata taarifa hizo, alishtushwa na kwamba hata nchi hiyo, watokayo raia hao ilishtuka pia, na kwamba kitendo hicho, pengine kiliweza kuleta utengano kwa namna aina ya tukio lililotokea.

Prof. Lipumba alisema jambo la kushangaza vyombo vya habari, viliripoti kuwa Jeshi la Polisi, lilikuwa limetoa taarifa ya awali ya kwamba kulinaswa mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mshtakiwa wa sakata hilo, Victor Kalist na raia hao wa kigeni.

"Kitendo cha kukamatwa raia wa kigeni, kiliwaaminisha watu kuwa walikuwa wanahusika, na pengeni kutokana na uzito wa tukio lenyewe ni wazi kuwa hata nchi yao itakuwa imeshtushwa pia kwa hiyo ni vyema Serikali ikaomba radhi kwakuwa hawana hatia," alisema Prof. Lipumba

Prof. Lipumba alisema jeshi la Polisi, linapaswa kuwa makini pia katika kufanya upelelezi wake, hususani katika matukio kama hayo, ili kuondoa mkanganyiko kama huo, ambao unaweza kuigharimu nchi kidiplomasia.

Alisema kuwa Jeshi hilo, pia linapaswa kuweka wazi utendaji kazi wake, huku akikumbushia matokeo ya uchunguzi wa matukio yaliyotokea Zanzibari, likiwamo tukio la mauji ya Padri Evarist Mushi.

Alitoa mwito pia kwa vyombo vya sheria vya Serikali, kuwa makini katika kuandaa mashtaka ili kuhakikisha kuwa vinatenda haki.

Kuhusiana na hilo, alitolea mfano iliyokuwa kesi ya Mwenyekiti wa Taasisi za Kiislamu, Shekh Issa Ponda, na kusema kuwa kulikuwa na makosa kuanzia kufunguliwa kwa kesi hiyo, kwa kuwa ilifunguliwa kijinai ilihali mazingira ya kesi hiyo, yalikuwa ya kesi ya madai.

Prof. Lipumba alizungumzia uchumi wa nchi, na kuitaka Serikali kuandaa mikakati ya kuikwamua nchi kutokana na kuporomoka kwa uchumi.

Alisema katika kipindi cha bajeti hii, ni vyema kukawekwa mipango ya kukamilisha miradi inayowekwa ikiwa ni pamoja na kutafuta vyanzo vya ndani vya fedha na kuachana na kasumba ya kukopa kwa nadharia kuwa Tanzania inakopesheka.

"Inashangaza kuona Serikali inajivua kabisa kuwa inakopesheka, na inatumia njia hiyo, kuendelea kukopa si sawa, tunapaswa kuwa na mipango madhubuti ya kukusanya fedha za ndani kupitia vyanzo vyetu vya rasilimali tulizonazo," alisema Lipumba.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.