NAIBU WAZIRI AINGILIA KATI UGOMVI WA LADY JAYDEE NA CLOUDS FM....RUGE AKIMBILIA MAHAKAMANI
Lady Jaydee
IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu
Waziri wa Habari Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani
kulivalia njuga suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media
Group Ruge Mutahaba na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady
Jaydee’ Ruge ametoa ya moyoni.
Tanzania Daima ambayo ilimpigia
simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada ya Makala kutamka kwamba
atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba na kuleta suluhu.
“Mimi kana nilivyosema katika
tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize pande
zote mbili hasa mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi
sasa Lady Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa
kumuelewa”
Na siyo Waziri Makalla tu pia
ikiwezekana hata kama kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika
kiti moto watuulize maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu
mimi niko radhi kufanya hivyo” anasema Ruge.
Wakati huohuo Ruge ameongeza
kwamba tayari ameshafuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungulia
jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo amepelekewa
msanii huyo akiitwa katika vyombo vya sheria.
Lakini ninaweza kusema jambo hili
linaweza kuzungumzika nje ya vyombo vya sheria kwani sisi tunaliona ni jambo
dogo na la mzaha lakini lina athari kubwa katika jamii inayotuzunguka anasema
Ruge.
Mwanzoni mwa mwezi huu Lady
Jaydee aliamua kuibuka na kuituhumu Clouds Media Group kwa kutumia mitandao ya
kijamii kama facebook, twitter nab log yake kwamba wana muhujumu kimuziki ,
kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge na kipaji chake kwa ujumba
tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
Mwandishi wa habari hii alijaribu
kumtafuta Lady Jaydee azungumzie kuhusu kauli ya Waziri kwa kupitia simu ya
mumewake Gadner Habash simu iliita bila kupokelewa. (chanzo MpekuziBlog)
Comments