NZERA AWA REDDS MISS KIBAHA

 Malkia wa Kibaha Nzera akiwa katika moja ya mapozi yaliyochangia kushinda taji hilo
 Redds Miss Kibaha Nzera Kitano (katikati) akiwa na mshindi wa pili Ester Albert (kushoto) na Rachel Joh aliyeshika nafasi ya tatu katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi mjini Kibaha, Pwani. (NA MPIGAPICHA WETU)




Na Mwandishi wetu

ALIYEKUWA mshiriki namba 6 katika shindano la kumsaka Redds Miss Kibaha 2013 Nzera  Kitano ameibuka kua Redds Miss Kibaha 2013 katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Conteainer  Kibaha Maili Moja mkoani Pwani.

Nzera ambae alionekana kuwa mchezi tangu mwanzo wa shindano aliweza kupenya katika hatua ya nusu fainali ambapo aliingia katika warembo watano bora kati ya washiriki 10 waliokuwa wakishindana kuwania taji hilo.

Aidha kwa ushindi huo  Nzera amepata zawadi ya fedha taslimu sh.300,000 pia amepa ofa ya kwenda kuchagua vipodozi na mapambo ya aina mbalimbali katika duka la Shear Illusion lilipo Mlimani City pamoja na king’amuzi kutoka kampuni ya Multichoice ambapo atafungiwa bure.

Mshindi wa pili ni Ester Albert ambaye amepata fedha taslimu kiasi cha sh.200,000 pia atapata ofa ya kulipiwa ada ya shule au kutafutiwa kazi na mdau ambaye hataki kutaja kwenye vyombo vya habari.

Mshindi wa tatu ni Rachel John aliyepata fedha taslimu sh. 150,000 huku nafasi ya nne ikienda kwa Sylvia John huku nafasi ya tano ilikwenda kwa Beatrice Bahaya.

Kwa ushindi huo warembo wote watano wamepata nafasi ya kwenda kushiriki kwenye shindano la Redds Miss Pwani watakakochuana na warembo wa Bagamoyo kuwania tiketi ya kwenda kushiriki katika shindano la Kanda ikiwa ni katika kuwania  tiketi ya shindano la taifa.
Shindano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO) na kudhaminiwa na
Redds Miss Kibaha ilidhaminiwa na Tanzania Distilleries Konyagi kupitia kinywaji cha Dododma Wine, Redds Premium Cold, Fredito Entertainment, CXC Africa, Michuzi Media Group |(MMG), Aco Catering & Servises, Pr Studio, ASET ,Santorine Holiday Resort na Amazon Night Club.

Bendi ya Muziki wa dansi ya Mashujaa ilitumbuiza na kuwachengua mashabi wa urembo wa mkoa wa Pwani.Washiriki wengine waliobaki walipata kifutajasho cha .sh.100,000 kila mmoja
Mwisho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.