REFA WA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI NI HUYU HAPA

Leslie Liunda

Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA MEI 14, 2013 SAA 9:5 ALASIRI
REFA Martin Saanya kutoka Morogoro ndiye atakayechezesha pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga SC la kufunga pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka nchini ili kujionea nani zaidi baina ya miamba hiyo, Saanya atasaidiwa na Samuel Mpenzu wa Arusha na Jesse Erasmo kutoka Morogoro, wakati refa akiba atakuwa ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam.
Kamisaa wa mechi hiyo atakuwa Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathmini wa waamuzi atakuwa ni Leslie Liunda wa Dar es Salaam.
Mashabiki watakaotaka kwenda kushuhudia mpambano huo wa mahasimu wa jadi katika soka ya Tanzania, watalazimika kulipa Sh. 5,000, hicho kikiwa kiingilio cha chini zaidi katika sehemu ya viti vya Rangi ya Bluu. 
Aidha, katika mchezo huo utakaoanza saa 10:00 jioni, viingilio vingine ‘nafuu kidogo’ vitakuwa ni Sh 7,000 kwa viti ya Rangi ya Kijani na Sh. 10,000 kwa viti vya Rangi ya Chungwa.
Upande wa ‘wakubwa’, viingilio vitakuwa ni Sh. 15,000 kwa VIP C, Sh. 20,000 kwa VIP B na Sh. 30,000 kwa VIP A.
Ofisa Haabri wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura amesema kwamba viingilio hivyo ni sawa na viingilio vya mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo baina ya miamba hao, Oktoba 3, mwaka jana. 
Wambura alisema tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo, yaani Ijumaa wiki hii katika vituo mbalimbali vitakavyotajwa.
Tayari miamba hiyo ya soka nchini iko mafichoni kwa maandalizi ya mpambano huo.
Yanga wameweka kambi yao kisiwani Pemba katika hoteli ya Samail mkabala na benki ya PBZ, wakifanya mazoezi Uwanja wa Gombani wakati Simba wameweka kambi maeneo ya Mbweni JKT Zanzibar wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung.
Wakati Yanga walitua Pemba Ijumaa jioni, mahasimu wao wa jadi, Simba SC waliwasili Zanzibar Jumapili jioni na mara moja kuanza kujifua kwa ajili mchezo huo, unaosubiriwa kwa hamu.    Kwa hisani ya Bin Zubeiry Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.