WARSHA YA WAZI KUJADILI MATOKEO YA UCHAMBUZI WA KINA WA MAENEO YA KIPAUMBELE YA KITAIFA
MGENI RASMI MHE. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA KIKWETE
Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (Ikulu) inawatangazia na kuwaalika wadau na wananchi wote kuhudhuria Warsha ya Wazi (Open Day) kupata maelezo, kujadili na kutoa maoni juu ya miradi na program zitakazotekelezwa na Serikali kwa kipindi cha miaka mitatu (2013/14 hadi 2015/16) katika maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12-2015/16). Miradi hiyo inatokana na uchambuzi wa kina uliofanywa na wataalamu wa kitanzania kwa kutumia mfumo mpya wa kimaabara (labs)
Huu ni mfumo ambao Serikali imeuanzisha ili kuhakikisha ushirikishwaji mpana wa wadau na wananchi kwa ujumla katika utekelezeaji wa miradi ya kipaumbele ya Kitaifa.
Warsha hiyo ya wazi itafanyika ijumaa tarehe 24/05/2013 katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar Es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Wote mnakaribishwa!

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano
Ikulu
DAR ES SALAAM

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.