BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI YAHAMIA OFISI MPYA

HESLB
HIGHER EDUCATION STUDENTS’ LOANS BOARD
TUNAHAMA
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawajulisha wadau wake wote kuwa Ofisi yake ya Makao Makuu inahama kutoka Jengo la TIRDO, Barabara ya Kimweri, Msasani kwenda  Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na. 46, Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge, Dar es Salaam kufikia Juni 30, 2013.
Katika kipindi cha kuhama, Bodi itahakikisha huduma zinarejea katika hali ya kawaida ndani ya siku chache.
Aidha uombaji wa mikopo kwa njia ta mtandao upo kama kawaida, na hivyo waombaji wa mikopo wanaweza kuendelea na utaratibu wa kuomba mikopo. Hata hivyo, huduma ya simu kwa waombaji wa mikopo imesitishwa kwa muda wakati mitambo ikifungwa na huduma itaendelea kama kawaida kuanzia Jumanne Juni 25, 2013
Bodi inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaotokea wakati ikijiweka sawa katika makazi mapya.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na.. 46, Barabara ya Sam
Nujoma,          Mwenge
S.L.P. 76068, Dar es Salaam, Tanzania.
Simu: +255 22 2669036/2669037 Faksi:  +255 22 2669039
Barua pepe: info@heslb.go.tz
Tovuti : www.heslb.go.tz

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.