Comments
HOYCE TEMU KATIKA SEMINA YA ‘HOW TO FIND YOUR DESTINY’
Mwendesaji wa semina ya “How To Find Your Destiny” Hoyce Temu akisikiliza utambulisho kutoka kwa washiriki waliohudhuria semina hiyo ambao
baadhi yao ni wajasiriamali, waajiriwa wa serikali, Mentors na
wanafunzi wa vyuo. Semina hiyo imefanyika kwenye Taasisi ya Mara
Foundation ya jijini Dar.
Pichani juu na chini ni Mwendeshaji wa semina ya “How To Find Your Destiny”
Hoyce Temu aki-share experience ya maisha yake mpaka hapo alipofika
baada ya kupitia vikwazo vingi, kuvuka mabonde na malima wakati wa
semina hiyo.
Pichani juu na chini ni Washiriki
wa semina ya “How To Find Your Destiny” wakifuatilia kwa umakini
shuhuda na mifano mbalimbali ya maisha iliyokuwa ikitolewa na
Mwendeshaji wa Semina hiyo Hoyce Temu(hayupo pichani).
Mwendeshaji wa Semina ya “How To
Find Your Destiny” Hoyce Temu akigawa kitabu chake kinachoelezea
historia ya maisha yake kinachoitwa "Nayakumbuka Yote" ambacho kinauzwa
katika maduka mbalimbali ya vitabu jijini Dar na Pesa inayopatikana
katika mauzo hayo asilimia 80 inakwenda kulipia ada za shule kwa
wasichana ambao ni mayatima na asilimia 20 inakwenda kwa mchapishaji.
Mmoja wa washiriki akimpongeza
Hoyce Temu kwa ujasiri aliokuwa nao na mateso aliyopitia katika maisha
yake mpaka kufikia hapo alipo.
Hoyce Temu akisaini autograph kwa mmoja washiriki.
Hoyce Temu akishow love na Mmiliki wa Beutylicious Saloon iliyopo Mikocheni B Irene Juliet Mbuya.
Pichani juu na chini ni Baadhi ya
washiriki wakipata picha ya ukumbusho na Mrembo wa zamani aliyewahi
kushika taji la Miss Tanzania mwaka 1999 Hoyce Temu.
Vijana jijini Dar es Salaam
wamepata fursa ya kushiriki katika semina iliyoandaliwa na Mikono
Business Consult kwa ajili ya kuwapa hamasa na kuwataka wasikate tamaa
ili wajipange na kuangalia nini wanachotaka kukifanya katika maisha yao.
Semina hiyo iliyoendeshwa na
Miss Tanzania wa zamani na Communication Analyst wa Umoja wa Mataifa
Tanzania Bi. Hoyce Temu ilifahamika kwa jina la “How To Find Your
Destiny” imeonekana kuwavutia washiriki waliohudhuria kutoka sehemu
mbalimbali.
Comments