*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA UJERUMAN ALIYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Ujeruman nchini Tanzania, Klaus Peter Brandes, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake, nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ujeruman nchini Tanzania, Klaus Peter Brandes, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.
**********************************
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatano Juni 12, 2013 amekutana na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Klaus Peter Blandes, ambaye amefika ofisini kwa Mheshimiwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga.
Balozi Blandes alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa katika kipindi chake kama Balozi nchini Tanzania, Ujerumani imeendelea kuwa mshirika mzuri wa Tanzania na kwamba anaamini alikuwa anaendeleza historia ya mahusiano mema ambayo Tanzania imekuwa nayo kwa miaka mingi.
Katika maeneo ambayo Ujerumani imekuwa katika uwekezaji Tanzania ni sambamba na eneo la Nishati ya umeme na usafirishaji ambapo tayari makampuni kadhaa ya Ujerumani yameonesha nia ya kuwekeza katika Reli ya Kati kwa lengo la kufungua soko kwa nchi za Afrika Mashariki. Pia, Ujerumani ina uwekezaji mkubwa katika sekta ya ujenzi hususani viwanda vya saruji.

Kwa upande wa Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Balozi Blandes kuwa amefanya kazi nzuri katika kuhamasisha mahusiano baina ya Tanzania na Ujerumani na kwamba katika kipindi chake akiwa Balozi hapa nchini, uhusiano wa Ujerumani kwa Tanzania umezidi kuimarika na mchango wa nchi hiyo katika shughuli mbalimbali za maendeleo nchini Tanzania ni kiashirio kizuri cha urafiki na udugu.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza pia Balozi Blandes kuwa, Ujerumani imeendelea kuwa rafiki wa Tanzania na sasa pia rafiki wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Balozi Blandes anasema; “Ujerumani inaitazama Afrika Mashariki kama eneo ambalo ni muhimu kwa uwekezaji na pia Tanzania inayo maeneo mengi ambayo yanaweza kuboreshwa na hivyo kuzidisha uzalishaji kwa soko la ndani na nje.”

Balozi Blandes anafafanua pia kuwa, Tanzania ina mengi ya kujivunia na ni nchi inayoheshimika sana duniani. “Mheshimiwa Makamu kama hapa kwenu wanakuja viongozi mbalimbali wakubwa wa Dunia mnachotakiwa kufanya ni kuendeleza pazuri mlipo ili nchi yenu ipate tija,” anasema.

Katika mkutano huo sambamba na Balozi Blandes kumshukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa ushirikiano aliompatia katika kipindi akiwa Balozi, pia Mheshimiwa Makamu wa Rais alimtaka Balozi Blandes kuendelea kuwa rafiki wa Tanzania kwa kutumia nafasi yake ya uwakilishi sambamba na yeye kama Balozi aliyefanya kazi vema hapa Tanzania.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.