REDD'S MISS KILIMANJARO MBIONI KUPATIKANA

                          Baadhi ya warembo wakiwa katika mazoezi


Warembo 12 wanaotarajiwa kupanda jukwaani Juni 15 mwaka huu kuchuana katika shindano la kumsaka malkia wa urembo mkoani Kilimanjaro, Redds Miss Kilimanjaro 2013 wameingia kambini leo.
Walimbwende hao wanaotarajia kupambana kumpata Mrithi wa Redds Miss Kilimanjaro 2012, Anande Michael anayeshikilia taji hilo kwa sasa, wameweka kambi katika hoteli ya Hugo, iliyoko nje kidogo ya mji wa Moshi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mratibu wa Mashindano hayo, Mkurugenzi wa Kampuni wa Rick Plan Company Ltd, Jackline Chuwa alisema ameamua kuwaingiza warembo kambini mapema ili kuhakikisha kuwa mashindano ya mwaka huu yanakuwa toofauti na ya mwaka jana.
“Warembo wanaingia kambini Le,  ili kuhakikisha kuwa mashindano yanakuwa ya kipekee, tuimeboresha mamnbo mengio na lengo ni kumpata Redds Miss Tanzania 2013, warembo wapo pale Hugo Hotel,” alisema Chuwa.
Mkurugenzi huyo alisema mashindano ya mwaka huu yatafanyika Juni 15 mwaka huu, kuanzia saa moja kamili jioni katikia ukumbi wa La Liga Carnivore na kuongeza kuwa viingilio ni sh. 15,000 kwa viti vya kawaida n ash. 30,000 kwa viti vya watu maalum (VIP).
Kuhusu Burudani, Mkurugenzi huyo aliwataja wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na JB, msanii wa kimataifa kutoka Burundi, Kidumu na Bendi yake, Ngoma za asili na Sarakasi huku mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe.
Redds Miss Kilimanjaro 2013 inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redds Original, Panone and Company Ltd, Bonite Bottlers kupitia kinywaji baridi cha Cocacola na maji ya Kilimanjaro, Mr. Price, Hugo Hotel na Kilimanjaro Express Bus.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.