ROSEMARY PETER AVISHWA TAJI LA REDDS MISS NYAMAGANA 2013, BAADA YAMSHINDI WA TAJI HILO DIANA AMIMO KUDANGANYA URAIA NA UMRI WAKE



Mkurugenzi wa Club Fusion wadhamini wa shindano la Miss Nyamagana 2013, Mr. George akipeana mkono na Redds Miss Nyamagana 2013 Rosemary Peter, mara baada ya kuvishwa taji hilo.


Redds Miss Nyamagana 2013/14 Rosemary Peter katika pozz, mara baada ya kutawazwa rasmi kushika taji hilo, katika hafla fupi iliyofanyika katika hotel ya New Mwanza ya kumvua aliyekuwa akishikila taji hilo Mrembo Diana Amimo baada ya kudanganya Urai wake na Umri.

---

Rosemary Peter, ni mshindi wa pili katika shindano la kumtafuta Redds Miss Nyamagana 2013, shindano lililofanyika tarehe 11/05/2013 katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza.

Alhamisi ya tarehe 06/06/2013, Rosemary peter amevishwa taji la Redds Miss Nyamagana 2013, baada ya Diana Amimo aliyekuwa mshindi wa taji hilo kudaganya Uraia na umri wake katika shindano hilo
Udanganyifu huo uligunduliwa na kuthibitishwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Mwanza, baada ya maafisa wake kumshikilia na kumuhoji mrembo huyo, wiki moja mara baada ya shindano hilo.

Kwa Mujibu wa kanuni na vigezo vya mashindano ya urembo hapa nchini, kuwa Msichana lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 18 hadi 24, Kampuni ya Stoppers Entertainment, imeweza kumvua taji mrembo Diana Amimo na kumvisha mshindi wa Pili Rosemary Peter kuwa Redds Miss Nyamagana 2013/14.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.