SUNDERLAND,SYMBION KUJENGA ACADEMY YA SOKA TANZANIA

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jioni hii, kuhusu moja ya mafanikio ya ziara ya kikazi ya Rais Jakaya Kikwete, Uingereza ambapo ameahidiwa na Klabu ya Sunderland ya Uingereza na Symbion ya Marekani kujenga Kituo kikubwa cha maendeleo ya mchezo wa soka nchini (Soccer Academy). Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa wizara hiyo, Leonard Thadeo. (PICHA NA KAMANDSA RICHARD MWAIKENDA)
Baadhi ya wanahabari wakiwa kazini





TAARIFA YA WAZIRI WA HABARI, VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO, DK. FENELLA MUKANGARA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UJENZI WA ACADEMY YA MPIRA WA MIGUU HAPA NCHINI

§        Kama mnavyofahamu, hivi karibuni Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa katika ziara yake ya kikazi nchini Uingereza.

§        Mhe. Rais alipokuwa nchini Uingereza alitembelea Club ya Sunderland. Mhe. Rais alihahidiwa kujengewa Academy ya Mpira wa Miguu na Kampuni ya Symbion Power ya Marekani ambayo itashirikiana na Club ya Sanderland katika kuindesha.

§        Hiyo Academy tunategemea itawezesha clubs zetu kupata wachezaji walio bora na walioandaliwa kuwa wachezaji wa taifa na kimataifa na hivyo kuboresha timu yetu ya Taifa na kuendelea kukuza muamuko wa masuala ya mpira wa miguu nchini.

§        Tunatarajia suala hili litafanyika na kutekelezwa mapema iwezekanavyo

§        Katika mpango  huo, Kampuni ya Symbion pia itajenga viwanja vya michezo (sports courts) pale Kidongo Chekundu. 

§        Kutokana na umuhimu wa suala hili, viongozi wakuu wa Kampuni ya Symbion wanatarajia kuja hapa nchini na nitakutana nao kwa ajili ya makubaliano mbalimbali na maandalizi ya utekelezaji.

§        Hivi sasa kama Serikali tunatafuta sehemu itakayojengwa Academy hiyo.  

§        Matarajio au nia yetu ni kujenga Academy hiyo Dar es Salaam au maeneo yaliyo karibu na Dar es Salaam.

§        Napenda nichukue fursa hii kumshukuru sana Mh. Rais kwa kufanikisha suala hili.

§         Napenda pia kumshukuru Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Zungu Azzan kwa kuwezesha kupatikana kwa viwanja vya Kidongo Chekundu.


§        Napenda pia kutumia fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru vijana wetu wa timu ya Taifa ”Taifa Stars” kwa juhudi na mchezo mzuri waliouonyesha wakati wa mechi yao na Timu ya Taifa ya Ivory Coast jumapili iliyopita.  Tupo pamoja nao na tutaendelea kuhakikisha tunawajengea uwezo zaidi ili waweze kupata mafanikio makubwa huko mbeleni.

§        Huko tunakoelekea, Academy itakuwa chimbuko la kupata wachezaji wazuri wa timu ya Taifa.



Asanteni kwa kunisikiliza

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.