Airtel Tanzania kutumia Milioni 150/- katika Mradi wa Vitabu wa 'Airtel Shule Yetu' kwa mwaka huu

 Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson  Mmbando akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam. Kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Bi. Hawa Bayumi na Kaimu Mkurugenzi Ukuzaji na Rasilimali wa Mamlaka ya Elimu (TEA), Bi. Sylivia Lupembe Gunze.
 *****************************
Kampuni ya Bharti ("Airtel") inayoongoza kwa kutoa huduma za mawasiliano katika nchi 20 barani Afrika na Asia leo imetangaza kutumia jumla ya milioni 150 katika mradi wa Airtel shule Yetu pamoja na shule 100 zitakazofaidika na mradi wa AIRTEL SHULE YETU utakaoziwezesha shule za sekondari nchini kupata vitabu vya kiada vitakavyowasaidi katika msomo na kuongeza kiwango cha ufaulu nchini.

Kupitia  droo maalum iliyoendeshwa na Airtel leo  Tanzania  Shule 100 kutoka katika mikoa mbalimbali nchini zimechaguliwa na kuingia katika mradi wa shule yetu kwa mwaka wa 2013 - 2014.

Akiongea wakati wa droo iliyofanyika katika makao makuu ya Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson  Mmbando alisema, kwa miaka 11 Mfululizo sasa Airtel chini ya mradi wetu wa "Shule yetu" tumeweza kuchangia katika sekta ya elimu na kuzifikia shule zaidi ya 950 na kutoa vitabu vyenye zaidi ya thamani ya shilingi bilioni 1.6  mpaka sasa.

"Tunafahamu jitihada za Serikali chini ya wizara ya elimu katika kupambana na changamoto hizi hivyo kuuungana na serikali katika kuinua sekta ya elimu kupitia mradi huu wa shule yetu ambao umeleta tija na kuleta mfanikio katika shule tulizoweza kuzifikia mpaka sasa.Tunaahidi kuendelea kuisaidi jamii kupitia miradi yetu mbalimbali tuliyonayo hususani katika elimu. Aliongea Mmbando

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi ukuzaji na rasilimali wa Mamlaka ya Elimu (TEA) Bi, Sylivia Lupembe Gunze ambae ndie aliyekuwa Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya kuchagua shule zitakazofaidika na mradi wa Airtel Shule yetu mwaka huu alisema "Tunaishukuru Airtel kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia sekta ya elimu nchini.

Tunazo changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo uhaba wa vitabu mashuleni ambapo kwa sasa uwiano wa viabu mashuleni ni kitabu kimoja kinatumika na wanafunzi 5 hivyo msaaada huu utasaidia sana kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika shule zinazofaidika nchini.

Zaidi ya changamoto za elimu kuna tatizo la uhaba wa madawati, madarasa, upungufu wa walimu hasa kwa maeneo ya vijijini, pamoja na ufahamu wa juu wa technologia mpya za ufundishaji mashuleni. Hivyo basi ninachukua fulsa hii kunawaomba makampuni mengine na wadau mbalimbali washirikiane nasi kuzitatua changamoto hizi na kuleta elimu bora katika taifa letu kwani vijana hao ni nguvu kazi ya kesho.

Kwa Upande wake Meneja huduma za jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi alisema" kwa mwaka huu tumewekeza kiasi cha shilingi milioni 150 katika mradi huu wa shule yetu lakini tunayo maeneo mengine ambayo tumejipanga kuyafanyia kazi kwa mwaka huu ikiwa ni pamoja na  kutoa msaada wa itechnologia kwa kutoa msaada wa computer mashuleni pamoja na kutoa elimu ya nadharia kwa wanafunzi wa kike na kuwawezesha kujitambua na kupata ujuzi utakaowapa ufanisi katika masomo yao na kujiwekea  malengo katika maisha yao ya baadaye"

Airtel Tanzania baada ya kutangaza shule hizi zitakazofaidika na mradi wa Airtel shule yetu zilizopo nchi nzima itaanza kavitawanya vitabu hivyo katika kila mkoa na wilaya ili viwafikie walimu, wanafunzi na maafisa elimu wa mikoa husika ili vitumike kutimiza malengo ya Mradi wa Airtel Shule yetu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.