GREEN WASTE PRO IKISHIRIKIANA NA VIONGOZI KATA YA KIVUKONI NA KANISA LA UNIVERSAL WAFANYA USAFI FUKWE YA OCEAN ROAD HADI AGA KHAN
Mtendaji wa kata ya Kivukoni Bw.
Renatus Ruhungu akizungumzia hatua yao ya kushirikisha wadau katika
zoezi la kufanya usafi manispaa ya Ilala, ambapo amesema mwezi ujao
wanajiandaa kushirikiana na wenzao wa Chuo cha IFM, ili vijana hao
waweze kuhamasika na suala la usafi na kuwa wataendelea kushirikisha
taasisi, vikundi na asasi mbalimbali ili zifahamu kuwa usafi ni jukumu
la kila mtu bila kuisahau kampuni ya usafi ilala ya Green Waste Pro ltd.
Katika zoezi hilo leo wameshirikiana na Kikundi cha vijana cha Youth
Power Group cha Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu kusafisha fukwe
ya Bahari ya Hindi kuanzia eneo la Ocean Road Hospital mpaka Aga Khan.
Mchungaji wa Kanisa la Universal la
Ufalme wa Mungu Marcos Braga akizungumza wakati wa zoezi la pamoja na
viongozi wa kata ya Kivukoni na Kampuni ya Green Waste Pro kufanya usafi
kutoka ufukwe wa Ocean Road hadi eneo la Aga Khan ambapo amesema ni
jukumu lao kuendeleza maisha ya baadae ya taifa letu, hivyo kila wakati
wanajitoa kushiriki miradi na kazi tofauti zitakazofanikisha kulikomboa
taifa kimaendeleo likiwemo suala la usafi wa jiji.
Ameongeza kuwa walichifanya leo sio
mwishi bali watakuwa wakifanya mara mbili kwa mwezi katika maeneo
tofauti hivyo ameomba ushirikiano kwa serikali na wadau mbalimbali.
Mchungaji Marcos Braga wa Kanisa la
Universal la Ufalme wa Mungu akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya
Kata ya Kivukoni kabla kuelekea eneo la tukio kwa ajili ya kushiriki
zoezi la kusafisha fukwe ya Bahari ya Hindi kuanzisha Ocean Road
Hospital mpaka Aga Khan.
Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Renatus
Ruhungu (aliyeketi) Afisa Usafi wa Manispaa ya Ilala Bw. Samuel Bubegwa
(na wa tatu kushoto), Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste
Pro ltd Bw. Abdallah Mbena (kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi
ya vijana wa kikundi cha Youth Power Group cha Kanisa la Universal la
Ufalme wa Mungu.
Wanakikundi cha Youth Power Group wa
Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu wakielekea kwenye fukwe za bahari
ya Hindi kwa ajili ya zoezi la usafi.
Vijana wa Youth Power Group wakiwa na
Bango lao linalohamasisha vijana kupinga matumizi ya madawa ya kulevya
kwenye Barabara ya Obama.
Picha juu na chini ni Mtendaji wa
Kata ya Kivukoni Renatus Ruhungu (mwenye kofia nyeusi) akishiriki zoezi
hilo na baadhi ya wanakikundi.
Bw. Said Mazingira wa Kampuni ya Green
Waste Pro Ltd. akishiriki zoezi hilo na Kikundi cha Youth Power Group
kutoka kata ya Gerezani.
Mchungaji Marcos Braga wa Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu akijumuika kwenye zoezi hilo na vijana wake.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya
Usafi ya Green Waste Pro Ltd akishirkiana na vijana wa Kanisa la
Universal La Ufalme wa Mungu wakati wa zoezi hilo.
Kazi imepamba moto.
Viongozi, walinzi shirikishi na baadhi
ya wananchi wa kata ya Kivukoni katika manispaa ya Ilala jijini Dar es
Salaam wakishirikiana na waumini takriban 100 wa kanisa la Uokovu na
Ufufuo la Kidongo Chekundu leo wameendesha zoezi la kufanya usafi kwa
kuokota takataka na kufagia kuanzia eneo la ufukwe wa Ocean Road hadi
eneo la Aga Khan sambamba na kampuni ya usafi katika manispaa hiyo ya
Green Waste pro Ltd.
Akizungumza na vyombo vya habari
Mtendaji wa kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu amesema kwa leo
wanashirikiana na wenzao wa Universal Church wa kata ya Gerezani na
wadau wengine pamoja na Kampuni ya Green Waste Pro lakini wakati
mwingine watashirikisha wadau wengine katika utaratibu wao wa kufanya
usafi kila wiki ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya waraka wa Mkurugenzi
na mkuu wa Mkoa.
Ameongeza kuwa wameona wakifanya wao
tu ile dhana ya kuwa usafi ni wa kila mtu watakuwa wameipoteza, hivyo
wakaona ni vyema sasa kushirikisha taasisi na jamii zilizo kwao na mbazo
ziko nje pia kuzialika kuja kushikiana na wao kufanya usafi ili
wananchi waone kumbe sio kazi ya serikali.
Naye wa Kiongozi wa kanisa la
Universal la Ufalme wa Mungu Mchungaji Marcos Braga amesema wao kama
kanisa wakiangalia nchi wanaona vitu vipi vinatakiwa kuendelezwa na nini
kinatakiwa kifanyike, hivyo wameamua kutoka nje kwenda kuendeleza mji
wao kwa kuanzia na usafi.
Amefafanua kuwa kikundi cha vijana wa
kanisa hilo kinashiriki katika shughuli mbalimbali ambazo zinaigusa
jamii moja kwa moja na pia tuna kampeni inayosema ‘Kijana Mwerevu Sema
hapana kwa Madawa ya Kulevya’ kwa kuwa vijana wengi wanaangukia katika
matumizi ya dawa hizo na kufanya maendeleo ya taifa la kesho kuwa duni
Na .
--
Zainul A. Mzige,)
Comments